Featured Kitaifa

WATHIBITI UBORA WA SHULE NCHINI WATAKIWA KUSIMAMIA UTEKELZAJI WA MIRADI YA ELIMU

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Eliamani Sedoyeka,akizungumza  wakati wa kufunga kikao kazi cha Viongozi, Maafisa Uthibiti Ubora wa Shule Makao Makuu na Wathibiti Ubora wa Shule Kanda na Wilaya Tanzania Bara kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Uthibiti Ubora upande wa Ualimu, Mathias Mvula,akielezea waliyojifunza katika kikao hicho  wakati wa kufunga kikao kazi cha Viongozi, Maafisa Uthibiti Ubora wa Shule Makao Makuu na Wathibiti Ubora wa Shule Kanda na Wilaya Tanzania Bara kilichofanyika jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani)  wakati wa kufunga kikao kazi cha Viongozi, Maafisa Uthibiti Ubora wa Shule Makao Makuu na Wathibiti Ubora wa Shule Kanda na Wilaya Tanzania Bara kilichofanyika jijini Dodoma.

Mthibiti Mkuu wa ubora wa Shule Halmashauri Chemba Bw. Amon Lembao,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki mara baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Eliamani Sedoyeka,kufunga kikao kazi cha Viongozi, Maafisa Uthibiti Ubora wa Shule Makao Makuu na Wathibiti Ubora wa Shule Kanda na Wilaya Tanzania Bara kilichofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja mara baada kufunga kikao kazi cha Viongozi, Maafisa Uthibiti Ubora wa Shule Makao Makuu na Wathibiti Ubora wa Shule Kanda na Wilaya Tanzania Bara kilichofanyika jijini Dodoma.

………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Eliamani Sedoyeka amewataka Wathibiti Ubora wa Shule nchini kufuatilia na kusimamia uwajibikaji wa Wakuu wa Shule kwenye fedha za miradi ya ujenzi wa shule zilizopelekwa na Serikali katika maeneo yao.

Amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa kufunga kikao kazi cha Viongozi, Maafisa Uthibiti Ubora wa Shule Makao Makuu na Wathibiti Ubora wa Shule Kanda na Wilaya Tanzania Bara.

Amesema kuna ujenzi wa miundombinu ya shule unaendelea ikiwemo kupitia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambapo amewataka kuhakikisha wanashiriki usimamizi wake na kutoa ushauri katika kuzingatia vigezo vya ubora vinavyohitajika kulingana na miongozo na Sera.

Aidha, amesema Serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza majukumu Wathibiti Ubora kwa kuongeza eneo la Uthibiti na ufuatiliaji kwa Vyuo vya Kati na Ufundi (VETA) ambavyo vinatarajiwa kuwepo katika kila Wilaya ifikapo mwaka 2025.

Amesema wathibiti ubora wa shule wanaweza kuisaidia Serikali katika kuhakikisha elimu bora yenye kuwasaidia vijana kupata maarifa, stadi na ujuzi inapatikana kwa kukagua vyema shule na vyuo vya ualimu.

Sedoyeka ameongeza kuwa Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika idara hiyo ikitambua kuwa wathibiti ubora ni mboni ya jicho ya elimu na amewahimiza wakasimamie ubora wa elimu kwa kuwa matokeo ya uthibiti ubora ni kuwepo kwa elimu bora huku akisisitiza suala la kuzingatia matumizi ya TEHAMAkatika utendaji.

“Ni wakati muafaka kufikiria ni namna gani mnaweza kuzifikia shule hata bila kufika physically ili kufanya ufuatiliaji,” amesema Prof. Sedoyeka.

Kwa upande, Mkurugenzi Msaidizi Uthibiti Ubora upande wa Ualimu, Mathias Mvula,amesema kuwa kikao hicho kimekuwa na tija kwa kuwa wamepata fursa ya kufanya tafakari ya pamoja kuona yale waliyoyapanga kama yametekelezeka na kupanga mikakati ya utendaji ili kuongeza ufanisi.

Awali Mthibiti Mkuu wa ubora wa Shule Halmashauri Chemba Bw. Amon Lembao,kwa niaba ya washiriki  amemshukuru Katibu Mkuu Sedoyeka kwa kuwezesha kikao hicho kwa kuwa mada zilizotolewa zimewapatia mahiri mbalimbali zitakazokwenda kuwasaidia katika utendaji.

About the author

mzalendoeditor