Na Lucas Raphael,Tabora
Jeshi la polisi mkoani Tabora linamshikilia Maria Matheo kwa tuhuma za kumuua mume Gabriel Nguwa (80) kwa kumkaba shingo hadi kifo wakati akiwa amelala.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Richard Abwao akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa alisema kwamba tukio hilo lilitokea mei 30 mwaka huu.
Alisema kwamba mnamo mei 30 mwaka huu majira ya saa 8 usiku kulitokea tukio la mauaji katika kitongoji cha Bugweda katika kijiji cha budushi kata ya Budushi wilaya ya nzega mkoani Tabora.
Kamanda huyo wa polisi alisema kwamba chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa muda mrefu kati ya wanandoa hao hususani nyati za jioni ,mwanamke anapolewa anakumtumu mumewe alikuwa ana msaada wowote katika maisha yao
Abwao alisema kwamba mbinu iliyotumika ni kumvizia mume akiwa amelala na kumkaba shingoni na kusababisha kifo chake.
Hata hivyo kamanda huyo wa polisi mkoani Tabora aliendelea kuwaeleza waandishi wa habari kwamba katika kipindi cha mei mwaka huu jeshi hilo walifanya msako na wakuwakata watuhumiwa 71 wa makosa mbalimbali .
Alisema kwamba katika makosa ya mauaji walikamatwa watuhumiwa 19 ,wizi watuhumiwa 31 watuhumiwa wa uvunjaji ni watu 17 na watuhumiwa 4 ni wa makosa ya kubaka.
Aidha jeshi hilo liliwakamata waganga 2 wasiokuwa na vibali katika kitongoji cha Lugange kijiji cha Gilimba kata ya Igulungu wilaya ya Uyui mkoani Tabora .
Abwao aliwataja waganga hao kuwa ni Yunge Kija (25) na Bundi Makomango (29)na kuongeza mnamo mei 31 majira ya saa 3 asabuhi katika kijiji hicho walikatwa watu hao wakifanya shughuliza uganga wakiwahawana vibali vya kufanyia kazi hiyo .