Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakjati
akifunga mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yamefungwa leo tarehe 30 Aprili, 2026 na yaliyofanyika kwa siku
tatu kuanzia tarehe 28 Aprili, 2026.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakjati
akifunga mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yamefungwa leo tarehe 30 Aprili, 2026 na yaliyofanyika kwa siku
tatu kuanzia tarehe 28 Aprili, 2026.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito
kwa watendaji wa uchaguzi kuhakikisha wanatumia muda wao kusoma Katiba, sheria
za uchaguzi, kanuni na maelekezo ya Tume ili waweze kusimamia uchaguzi kwa
weledi.
Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk
Salim Mbarouk Mkoani Morogoro leo tarehe 30 Aprili, 2026 wakati akifunga
mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 28
Aprili, 2026.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mchakato wa
maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Ismani Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa, Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara unaotarajiwa
kufanyika tarehe 01 Juni, 2026.
“Natumia nafasi hii kuendelea kuwasisitiza
kuhusu umuhimu wa kutenga sehemu ya muda wenu kusoma Katiba, sheria na
maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ili yawaongoze katika kusimamia
uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki,” amesema Jaji Mbarouk.
Amewataka watendaji hao wa uchaguzi
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi ili kufanikisha uchaguzi huo mdogo
ambao unafanyika kujaza nafasi wazi ya mbunge na madiwani.
“Jukumu
lililopo mbele yetu ni kubwa na muhimu, linahitaji umakini na kujituma. Ni
matazamio ya Tume kwamba, baada ya kupatiwa mafunzo haya, mtatekeleza majukumu
yenu kwa ufanisi na weledi mkizingatia ratiba ya utekelezaji ili kufanikisha
uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Ismani na Kata 12 za Tanzania Bara
unaotarajiwa kufanyika tarehe 01 Juni, 2026,” amesema Jaji Mbarouk.
Amesisitiza kuwa ili ufanisi uwepo ni muhimu
watendaji hao wazingatie sifa na uwezo wakati wa kuteua na kuajiri watendaji wa
vituo vya kupigia kura kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na
kuhesabu kura vituoni.
“Kuhusu ajira za watendaji wa vituo, tunayo
imani kuwa mtateua na kuajiri watendaji wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hii
muhimu kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura
vituoni. Kazi ambayo inahitaji umahiri, umakini na weledi katika kuitekeleza.,”
amesema Jaji Mbarouk.
Amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa
mafunzo ya watendaji wa vituo yanafanyika kwa ufanisi na weledi katika tarehe
zilizopangwa kwenye ratiba ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga
kuwajengea uwezo ili waweze kufahamu majukumu yao na kuyatekeleza ipasavyo
wakati wa uchaguzi.
Mafunzo hayo yamewahusisha Waratibu wa
Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi
Ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata, Maafisa Uchaguzi, Maafisa
Ununuzi na Wahasibu.
Kata 12 za Tanzania Bara zitakazofanya
uchaguzi wa Udiwani ni Mzimuni iliyopo Manispaa ya Kinondoni; Zongomera,
Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji wa Nzega; Ketare, Halmashauri ya
Mji wa Tarime na Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji
wa Kasulu.
Nyingine ni kata ya Kala iliyoko Halmashauri
ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya
Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe; Namasakata
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru; Bwongera, Halmashauri ya Wilaya ya Chato na
Kibiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Sehemu ya watendaji wa uchaguzi katika jimbo la
Isimani Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania bara wakisikiliza hotuba ya
kufunga mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 28
hadi 30 Aprili, 2026.
Sehemu ya watendaji wa uchaguzi katika jimbo la
Isimani Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania bara wakisikiliza hotuba ya
kufunga mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 28
hadi 30 Aprili, 2026.
Sehemu ya watendaji wa uchaguzi katika jimbo la
Isimani Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania bara wakisikiliza hotuba ya
kufunga mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 28
hadi 30 Aprili, 2026.







