Featured Michezo

SHAKA AWAAGA TEMBO WORRIORS,AMPONGEZA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KATIKA MICEZO

Written by mzalendoeditor
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka akisalimiana na Viongozi wa Timu ya Soka ya Watu Wenye Ulemavu (Tembo Worriers) , alipotembelea kambi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwaaga wachezaji kabla ya kwenda katika michuano hiyo.
Katibu Mkuu Mkuu TAFF Akizungumza wakati wa hafla ya  kuwatia moyo na kuwaaga wachezaji wa Timu ya Soka ya Watu Wenye Ulemavu (Tembo Worriers) kabla ya kwenda katika michuano hiyo walipotembelewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu (TAFF), Ndg. Peter Sarungi wakati akimkaribisha Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, aliyetembelea kambi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwaaga wachezaji kabla ya kwenda katika michuano hiyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Viongozi wa Timu ya Soka ya Watu Wenye Ulemavu (Tembo Worriers) , alipotembelea kambi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwaaga wachezaji kabla ya kwenda katika michuano hiyo.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI/CCM)
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka akikabidhiwa Cheti na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu (TAFF), Ndg. Peter Sarungi,Cha Shukrani kwa Niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa  kuipa timu hiyo sh. milioni 150 kwa ajili ya maandalizi na kugharamia kambi ya timu hiyo katika hotel ya Regency jijini Dar es Salaam, 
………………………………………..
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema matokeo na mwendo mzuri wa michezo hususan kwa timu ya Soka ya Watu Wenye Ulemavu (Tembo Worriors) ni matokeo ya utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
 
Shaka ameyasema hayo aliposhiriki hafla ya kuiaga Tembo warriors inayoelekea nchini Poland kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea mashindano ya dunia yatakayofanyika nchini Uturuki, hafla ambayo imefanyika katika Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam, ambapo alimpongeza Rais Samia kwa mageuzi makubwa anayoyafanya katika kada ya michezo kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
 
“Sisi kwenye Chama na hata Mwenyekiti wa Chama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wote mnafahamu kwamba dira yake mwelekeo wake unakwenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, ya mwaka 2020-2025. Kwenye Ilani huu na ninyi pia mmo kwenye yale ambayo katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. 
 
“Ninayo furaha kutamka kuwa kazi ya utekelezaji wa mkataba huu baina ya Chama Cha Mapinduzi na Watanzania inakwenda vizuri sana. Mageuzi makubwa ya kiuchumi inayopiga nchi yetu, lakini mageuzi makubwa kijamii inayopiga nchi yetu ni matokeo bora kabisa ya Ilani yenye viwango ya Chama Cha Mapinduzi.
 
“Nataka nichukue fursa hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Samia Suluhu Hassan kwa mageuzi makubwa anayoyafanya katika kada hii ya michezo nchini, lakini kwa uthubitu alionao,” amesema.
 
Shaka aliitaka timu hiyo kuitumia vyema imani waliyoonyeshwa na Rais Samia huku alisisitiza hana shaka kwamba itafanyia vizuri katika michuano hiyo.
 
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu (TAFF), Peter Sarungi alimshukuru na kumwahidi Rais Samia Suluhu Hassan kuwa timu hiyo inakwenda kufanya vizuri katika michuona ya Soka ya Dunia.
 
Amesema hatua ya Rais Samia kuipa timu hiyo sh. milioni 150 kwa ajili ya maandalizi na kugharamia kambi yake katika hotel ya Regency jijini Dar es Salaam kwa takriban miezi saba, imeonyesha jinsi anavyotaka mafanikio ya timu, hivyo wanamwahidi makubwa.
 
“Kwa namna ya kipekee mwaka jana mheshimiwa Rais alimwagiza mheshimiwa Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) kuja kutuchangia sh. Milioni 150 kwa ajili ya michezo yetu, lakini vilevile hatuwezi tukasahau kwamba amekuwa karibu sana na sisi, baada tu kushinda kwenda kombe la dunia alitualika kwenda Ikulu na akawa ametupa maelekezo na hayo ni maelekezo ya kwanza kabisa katika historia ya michezo. Timu ya Taifa kukaa kambini chini ya usimamizi na ufadhil wa serikali kwa zaidi ya miezi saba.
 
“Lakini vilevile nitambue na nikupe taarifa kuwa kwenye Kambi hii tuna timu ya Taifa ya walemavu wanaokwenda kushiriki michuano ya Jumuiya ya Madola, hawa wanatokea TPC (Tanzania Paralempic Committee) wapo wachezaji wawili.
 
“Mheshimiwa Rais alituagiza kwamba moja ya jambo ambalo angependa kuliona ni kuitangaza nchi yetu kupitia michezo, lakini vilevile kuhakikisha tunarudi na ushindi, na ushindi kwetu tulivyou ‘udefine’ (tafsiri) ni nafasi zile tatu za juu ambazo lazima urudi na medali, kombe na vitu vingine. Kwa hiyo, hiyo ni ‘target’ ambayo sisi tumepewa na kila siku tukilala tukiamka tunawaza hilo jambo na kuhakikisha tunailetea Tanzania heshima yake inayostahili. 
 
Sarungi amesema wananmshukuru Rais Samia kwa kuwa ameonyesha ni kiongozi na mama mlezi ambaye amekuwa faraja kubwa kwao.
 

About the author

mzalendoeditor