Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AKABIDHIWA MSAADA WA VIFAA TIBA NA DAWA KUTOKA KWA MADAKTARI BINGWA WA JAMHURI YA WATU WA CHINA WANAOTOA HUDUNA ZA AFYA KATIKA HOSPITALI ZA UNGUJA NA PEMBA

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Madaktari Bingwa kutoka Kichina wakiongozwa na Dr. Qu Lishuai (kulia kwa Rais) alipowasili katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, walipofika kwa ajili ya mazungumzo na kukabidhi Vifaa Tiba kwa ajili ya Hospitali za Mnazi Mmoja,Kivunge,Chakechake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Kiongozi wa Madaktari Bingwa kutoka Kichina Dr. Qu Lishuai akizungumza na kuwatambulisha Madaktari Bingwa wanaotowa huduma za afya katika Hospitali za Unguja na Pemba, wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa Tiba , hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Kiongozi wa Madaktari Bingwa kutoka China Dr.Qu Lishuai wakati akikabidhi Vifaa Tiba kwa ajili ya matumizi ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Unguja,Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,Chakechake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 7-6-2022. (Kulia kwa Dr Qu ) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Madaktari Bingwa wa Kichina wanaotoa huduma za Afya katika Hospitali za Unguja na Pemba, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kukabidhi Vifaa Tiba na Dawa mbalimbali kwa ajili ya Hospitli ya Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,Chakechake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar 

WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akizungumza wakati wa kukabidhiwa kwa Vifaa Tiba na Dawa kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Jamhuri ya Watu wa China, wanaotowa huduma za Afya katika hospitali za Unguja na Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Madaktari Bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China.(hawapo pichani)wanaotoa huduma za Afya katika Hospitali za Unguja na Pemba, walipofika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na kukabidhi Vifaa Tiba na Dawa mbalimbali kwa Hospitli ya Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja,Chakechake Pemba na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 7-6-2022, na (kushoto kwa Rais) ni baadhi ya Vifaa Tiba alivyokabidhiwa kwa ajili ya Hospitali za Zanzibar.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor