MWAKILISHI wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk.Charles Mhina,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Kutoa Maoni Kuhusu Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliofanyika leo Juni 2,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk.Charles Mhina ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa Kutoa Maoni Kuhusu Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliofanyika leo Juni 2,2022 jijini Dodoma.
Afisa Tawala Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi.Wamoja Ayubu,akielezea lengo la Mkutano wa Wadau wa Kutoa Maoni Kuhusu Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliofanyika leo Juni 2,2022 jijini Dodoma.
MWAKILISHI wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk.Charles Mhina,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa Wadau wa Kutoa Maoni Kuhusu Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliofanyika leo Juni 2,2022 jijini Dodoma.
………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
WADAU wa sekta ya Mifugo na Uvuvi wamekutana Jijini Dodoma kutoa maoni kuhusu rasimu ya mkataba wa huduma kwa wateja huku wakipendekeza mambo mbalimbali.
Akizungumza leo Juni 2 2022,jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Wadau wa Kutoa Maoni Kuhusu Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja ,Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dk.Charles Mhina, amesema mkataba huo ni muhimu kwani unawasaiodia kwenye kujiendesha kiweledi.
“Uadilifu weledi na uwajibikaji tunatakiwa kwenda katika misingi ambayo inazingatia kanuni za utumishi wa uuma.Kwenye eneo la weledi ni lazima kuwe na viwango vya huduma bora kama taasisi ndipo pale tunapopambanua kuwafikia wateja wetu kila kundi linamatarajio yake.
“Ukiwa shambani kwako tunakuhudumia kwa huduma za ugani tunahakikisha tunakufikishia kwa wakati na kwenye mifugo hivyo hivyo.Hata kwenye masoko tunafanya hivyo hivyo pamoja na huduma za vibali haya yote yanagusa katika weledi.
“Ili uwe na huduma bora ni lazima tuwe na uwajibikaji na ni lazima tuwekeane viwango ni namna gani tutawajibika kwa mteja wetu,”amesema.
Amesema wana matarajio makubwa watafikia malengo ya kutoa huduma bora ambazo zitaleta mabadiliko makubwa.
“Ninaamini tutafikia viwango na huduma zitaweza kuwafikia watu wengi tunafanya mapitio ya mkataba uliandaliwa tangu mwaka 2014 hivyo kuna mabadiliko mengi ambayo yametokea.Kuna mabadiliko ya kiteknolojia tulikuwa katika analogy lakini sasa hivi tunatoa vibali kwa kutumia Tehama,”amesema.
Kwa upande wake Afisa Tawala Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi.Wamoja Ayubu, ambaye pia ni mratibu wa rasimu ya mkataba kwa mteja amesema mkataba huo unaelezea namna ambavyo mteja anaweza kurejesha mrejesho wa huduma ambayo amepata.
“Mchakato huu ulianza tangu mwezi Marchi Katibi Mkuu aliunda timu ambayo ilikaa na kupitia na tulitoka na rasimu na Mei iliwasilishwa kwenye Wizara na mapendekezo yalitolewa sasa rasimu tumekuja kuwasilisha kwa wadau.
“Popote pale watakapotaka kuboresha tutayajadili kwa kuzingatia utendaji na sheria na taratibu michakato yake inazingatia sheria baada ya rasimu kukamilika tutaenda katika utekelezaji,”amesema.
Amesema mkataba huo ni muhimu kwani unapima utendaji wa taasisi ambapo wateja wataweza kuwapima kama wanafikia vile viwango.
Naye,Afisa Uhusiano na Masoko kutoka Kampuni ya Kilimanjaro International heather Industrie (KLIC) Fredrick Njoka amesema wamehudhuria mkutano huo kama wanufaikaji na wanataka kuhakikisha Wizara inakuwa na mikakati ambayo inawanufaisha wao.
“Zile changamoto ambazo tulikuwa tunaziona tunazitoa hapa hili ni jambo shirikishi na muhimu nah ii ndio sehemu pekee ya kuelezea kuna vitu vingi ambavyo tunataka viongezeke,”amesema