Featured Michezo

COASTAL UNION YAICHAPA AZAM FC NA KUTINGA FAINALI YA FA

Written by mzalendoeditor

HATIMAYE Timu ya Coastal Union imetinga  Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC baada ya kuiondosha Azam FC kwa mabao 6-5 kwa Mkwaju wa Penalti mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mchezo huo umepelekea kwenda hatua ya Matuta baada ya dakika 120 timu zote kutoka sare ya bila kufungana katika hatua hiyo Coastal union wameibuka na ushindi wa Penalti 6-5.

Sasa Coastal Union atacheza na Yanga Fainali ambao walimtoa Simba kwa bao 1-0 lililofungwa na Feisal Salum kwa shuti kali mechi iliyopigwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Fainali ya Michuano hiyo itachezwa Julai 2,2022 uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

About the author

mzalendoeditor