Featured Kitaifa

OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI YAOKOA TRILIONI 10 ZILIZOKUWA ZILIPWE KWA WATU WASIOSTAHILI

Written by mzalendoeditor

Wakili Mkuu wa serikali , Gabriel Malata akizungumza katika ufunguzi  wa mafunzo hayo jijini Arusha leo

Katibu Mkuu wizara ya Katiba na sheria ,Mary Makondo akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Jijini Arusha 

 Baadhi ya mawakili wa serikali wakiwa katika mafunzo mkoani Arusha.

………………………………………

NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Wakili Mkuu wa Serikali Mhe. Gabriel Malata amesema tangu kuanzishwa kwa ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mwaka 2018 wamefanikiwa kuokoa zaidi ya  Trillion 10 za serikali ambazo zingelipwa kwa watu wasio stahili kama serikali ingeshindwa mashauri.
Malata aliyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya mawakili wa serikali yaliyoanza leo Mei 23,2022 Jiji Arusha ambapo alisema kuwa kama serikali ingeshindwa mashauri hayo ingewajibika kuwalipa wadai fedha hizo na kushindwa kutoa huduma na kukuza uchumi kupitia fedha hizo.
Alieleza kuwa pamoja na   mafanikio pia wamefanikiwa kurejesha mali za serikali zilizochukuliwa na watu ambao wasio na nia  njema na serikali ambapo  lakini pia wameweza  Kutatua na kupunguza mrundikano wa mashauri kwa njia ya majadiliano pamoja na kupunguza migogoro.
“Tumeendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa weledi kwa niaba ya serikali ikiwa ni pamoja na kushiriki katika ukuzaji wa sheria nchini kupitia uendeshaji wa mashauri mahakamani ikiwemo mashauri ya madai, Katiba, haki za binadamu na usuluhishi,”Alisema.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo akifungua mafunzo hayo aliwataka mawakili wa serikali wote nchini kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao, kufanya kazi kwa bidii, umakini na uzalendo kwani wanamchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi.
Alisema kuwa Ofisi hiyo imechangia  katika uokoaji wa mapato ya serikali kwa kuisaidia kutolipa fidia  ya zaidi ya trilion kumi ambazo zingelipwa na mashauri ambayo yapo ndani na nje ya nchi ambayo kutokana na migogoro mbalimbali inayoibuka katika utekelezaji wa mikataba serikali inashtakiwa na kudaiwa fidia. 
“Tunatambua wajibu wa serikali ni kuwapatia  watumishi wake mafunzo hivyo dhumuni la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo mawakili wa serikali wote nchini,”alisema  Makondo.
Makondo alisema ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imefungua mfumo mahususi wa kuwatambua mawakili wa serikali na wanasheria wote utawawezesha kufanya kazi kwa weledi,bidii na uzalendo katika kuijenga nchi na kuchangia katika kuokoa madai ambayo yasipoendeshwa vizuri serikali italipa fidia kubwa.
“Fedha hizo zikiokolewa zinarudishwa katika mfumo mkuu wa serikali na kutumika katika maendeleo ya nchi na huduma zake kwa ujumla kama elimu,ujenzi wa miundombinu, sekta ya afya na kuchangia katika ujenzi wa nchi yetu,”alisema  Katibu Mkuu huyo.
Jenipher Kaaya ni Wakili wa Serikali mwandamizi alisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo,weledi na kijiamini katika kushindana na mawakili wenzao mahakamani endapo wakishtakiwa  watakuwa na nguvu kubwa kuliko ya awali katika kuwasilisha hoja zao za kisheria.
Hata hivyo mafunzo hayo ni juu ya uendeshwaji wa mashauri pamoja na upatanishi usuluhishi lengo ni kutambua umuhimu wa mawakili wa serikali katika kuchangia uandaaji wa nyaraka ipasavyo katika taasisi zote za serikali,usimamizi na uendeshwaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali au serikali yenyewe yakisimamiwa na wakili mkuu wa serikali.

About the author

mzalendoeditor