Featured • Kitaifa

TANZANIA YASISITIZA UENDELEZAJI WA MAGEUZI YA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA

Written by Alex Sonna

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha mageuzi katika usimamizi wa fedha za umma, kupitia msaada wa kiufundi unaotolewa kupitia Mpango wa Good Financial Governance (GFG III), wakati wa Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Ujerumani nchini, Bi. Julia Kronberg, akieleza kuwa Mpango wa Good Financial Governance (GFG) Tanzania umeelekeza nguvu katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato, udhibiti wa matumizi ya fedha za umma na kuimarisha uwazi katika sera za fedha, wakati wa Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Kamishna Msaidizi wa wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Melckzedeck Mbise, akitoa utaratibu wa majadiliano wakati wa Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma, ukihusisha wadau kutoka Ujerumani, Uswisi na Umoja wa Ulaya. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba, akieleza namna Mamlaka hiyo ilivyotekeleza  Mpango wa Good Financial Governance (GFG III), wakati wa Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Baadhi ya Wadau kutoka Wizara ya Fedha, taasisi za Serikali zinazotekeleza Mpango wa Good Financial Governance (GFG III), pamoja na washirika wa maendeleo kutoka Ujerumani, Uswisi na Umoja wa Ulaya  wakiwa katika Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Afisa Mwandamizi kutoa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Bw. Felix Kapesula, akitoa maelezo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla na washirika wa Maendeleo kutoka Ujerumani, Uswisi, Umoja wa Ulaya wakati wa Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla na washirika wa maendeleo  kutoka Ujerumani, Uswisi na Umoja wa Ulaya wakisikiliza maelezo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati wa Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla akisalimiana na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans baada ya Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla, akiwa katika picha ya pamoja na Meza Kuu wakati wa Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla (katikati),Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans (wa pili kushoto) na Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Ujerumani, Bi. Julia Kronberg, wakiwa katika picha ya pamoja na washirika wa Maendeleo kutoka Ujerumani, Uswisi, Umoja wa Ulaya wakati baada ya Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Wadau kutoka Zanzibar walioshiriki katika Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya  kumalizika kwa mkutano huo. 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Na. Peter Haule na Jordan Mbwambo, WF, Dodoma.

Serikali ya Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha mageuzi katika usimamizi wa fedha za umma, ikieleza kuwa msaada wa kiufundi unaotolewa kupitia Mpango wa Good Financial Governance (GFG III) unaofadhiliwa na washirika wa maendeleo kutoka Ujerumani, Uswisi na Umoja wa Ulaya unapaswa kutafsiriwa kuwa mifumo imara, uwezo endelevu wa taasisi na matokeo yanayopimika.

Msisitizo huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Asha Khamis Abdulla wakati wa Mkutano wa Kamati ya Usimamizi ya GFG III uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Mtumba, Dodoma.

Alisema GFG III imechangia katika maeneo mbalimbali muhimu, yakiwemo uhamasishaji wa mapato ya ndani, udhibiti wa matumizi ya umma, uwazi katika sera za fedha pamoja na mageuzi ya usimamizi wa fedha za umma Zanzibar.

Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa ni kuimarishwa kwa uwezo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), taarifa za matumizi ya kodi, mifumo ya kodi, uboreshaji wa ukaguzi na mageuzi ya manunuzi ya umma.

“Kwa kipindi kilichosaliacha utekelezaji wa Program hiyo hadi Julai 2027, msisitizo umewekwa katika kukamilisha shughuli ambazo bado hazijatekelezwa na kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanaingizwa kikamilifu katika mifumo ya Serikali“, alisema Bi. Abdulla.

Bi. Abdulla ilisisitiza umuhimu wa kuunganisha mageuzi yanayoungwa mkono na GFG III na vipaumbele vya taifa, ikiwemo Dira 2050, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV), Mkakati wa Muda wa Kati wa Mapato na Mpango mpana wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma.

Aidha, alisema kuwa awamu ijayo ya ushirikiano, maeneo yanayopendekezwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia za kidijitali na uchambuzi wa takwimu katika ukusanyaji wa mapato, sera za kodi, ukaguzi wa ndani, manunuzi ya umma, ubia kati ya Serikali na sekta binafsi, bajeti rafiki kwa mazingira, matumizi ya akili bandia na kuimarisha usimamizi wa fedha za umma Zanzibar.

Alisema ushirikiano wa baadaye unapaswa kuwa wenye kulenga matokeo, unaomilikiwa na taasisi za Serikali na unaozingatia uendelevu, ili mifumo, maarifa na zana zitakazotengenezwa ziendelee kutumika hata baada ya kumalizika kwa kipindi cha msaada wa GFG.

Mkutano huo umeweka msingi wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na washirika wake wa maendeleo katika kujenga mifumo bora ya usimamizi wa fedha za umma, kuongeza uwazi na uwajibikaji, pamoja na kuhakikisha rasilimali za umma zinakusanywa na kutumika kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Ujerumani, Bi. Julia Kronberg alisema kuwa Mpango wa Good Financial Governance (GFG) nchini Tanzania umeelekeza nguvu katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato, udhibiti wa matumizi ya fedha za umma na kuimarisha uwazi katika sera za fedha, huku washirika wa maendeleo wakitaka matokeo ya vitendo katika kipindi cha miezi 12 iliyosalia.

Alisema kuwa Mpango huo wa GFG unaoungwa mkono na Ujerumani, Uswisi na Umoja wa Ulaya na umekuwa ukitekelezwa nchini tangu mwaka 2016, ukijikita katika maeneo manne makuu ambayo ni uhamasishaji wa mapato, udhibiti wa matumizi ya umma, sera za fedha zinazotegemea ushahidi pamoja na kujenga uwezo wa usimamizi wa fedha za umma Zanzibar.

Katika mapitio ya mpango huo, washirika walieleza mafanikio kadhaa, likiwemo jukumu la GFG katika kusaidia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuandaa Mpango Mkakati wa Saba wa Shirika, kwa kutumia ushahidi na uzoefu wa utekelezaji wa mpango uliotangulia.

Takwimu zilizowasilishwa zinaonyesha kuwa usajili wa makundi hayo umeongezeka kutoka takribani 1,300 hadi zaidi ya 33,500 mwaka 2026, huku yakifanikiwa kupata zabuni za umma zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 67.

Hata hivyo, washirika wameainisha maeneo manne yanayohitaji kupewa kipaumbele katika kipindi kilichosalia, maeneo hayo ni kuongeza usajili wa wafanyabiashara wadogo na matumizi ya Electronic Fiscal Devices (EFD), kuimarisha uwazi wa masuala ya fedha, kuongeza ushirikishwaji wa wadau wakiwemo asasi za kiraia na kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji wa Ulaya nchini.

Washirika wamehimiza mazungumzo ya wazi na ya kujenga pamoja na kuweka hatua, majukumu na muda wa utekelezaji unaoweza kupimika, lengo ni kuhakikisha kipindi kilichobaki kinazalisha matokeo yanayoonekana na kuweka msingi wa uendelevu wa mageuzi baada ya awamu hiyo kukamilika.

Mkutano huo uliikutanisha Wizara ya Fedha, taasisi za Serikali zinazotekeleza mpango huo, pamoja na washirika wa maendeleo kutoka Ujerumani, Uswisi, Umoja wa Ulaya na GIZ, lengo lilikuwa kutathmini maendeleo na mafanikio ya GFG III, kubaini changamoto, kutoa mwelekeo wa kimkakati kwa kipindi kilichosalia na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na washirika wa maendeleo.

About the author

Alex Sonna