Featured Kitaifa

MHE. LUSWETULA ABAINISHA FURSA AKIWAKARIBISHA WAWEKEZAJI TANZANIA

Written by Alex Sonna


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akichangia hoja kuhusu uwekezaji katika sekta ya afya wakati wa Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha Afrika kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya, linalofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akiteta jambo na Waziri wa Fedha wa Sierra Leone, Mhe. Foday Kamara, wakati wa Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha Afrika, kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya, linalofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) (katikati), akiwasili katika Hoteli ya JW Marriott, Nairobi, Kenya, kushiriki Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha Afrika, kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya. Wengine ni wajumbe kutoka Tanzania.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akiteta jambo na Waziri kutoka Uganda, Mhe. Shartsi Musherure, wakati wa Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha Afrika, kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya, linalofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akifuatilia majadiliano wakati wa Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha Afrika, kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya, linalofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Wajumbe wa Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya wakiwa katika mkutano, jijini Nairobi, Kenya.

Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakishiriki Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya, linalofanyika jijini Nairobi, Kenya.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Na. Peter Haule, WF, Nairobi, Kenya

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), amewakaribisha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya afya Tanzania, akisema nchi ina sera thabiti zinazotabirika pamoja na mazingira salama na rafiki kwa uwekezaji.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), Mhe. Luswetula ametoa mwaliko huo wakati akichangia hoja katika Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika sekta ya afya, lililofanyika katika Hoteli ya JW Marriott, Nairobi, Kenya.

“Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya afya, pamoja na sera imara na zinazotabirika zinazoambatana na mazingira bora ya uwekezaji na usalama. Kinachohitajika ni kufuata sheria za nchi ili uwekezaji uwe na manufaa kwa mwekezaji na Watanzania kwa ujumla,” alisema Mhe. Luswetula

Akizungumzia mkutano huo Mhe. Luswetula alisema majadiliano katika jukwaa hilo yalilenga kujadili mikakati ya kuongeza mapato ya ndani kwa ajili ya kugharamia huduma za afya, utekelezaji wa ahadi za pamoja za ufadhili pamoja na kuweka sera na mazingira wezeshi yatakayochochea uwekezaji katika sekta hiyo.

Alisema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kuweka mazingira yanayowezesha upatikanaji na utoaji wa huduma bora za afya, hatua ambayo inatoa fursa zaidi kwa sekta binafsi kushiriki katika maendeleo ya sekta hiyo.

Aidha, alisema Tanzania imeendelea na utekelezaji wa programu ya Bima ya Afya kwa Wote, huku Serikali ikiwekeza kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya nchini.

Alisema uwepo wa mfumo mpana wa bima ya afya unatarajiwa kuwa na mchango katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na kuwawezesha wananchi kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli zao za maendeleo.

Vilevile alisema kuwa majadiliano hayo yalihusu matumizi ya mbinu bunifu za ufadhili na mifumo ya kuchanganya vyanzo mbalimbali vya fedha ili kuongeza rasilimali zinazohitajika katika kuboresha huduma za afya.

Mkutano huo uliowakutanisha Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali za Afrika zilizosaini Hati za Makubaliano (MoU) na Serikali ya Marekani kuhusu ufadhili wa sekta ya afya ulihudhuriwa pia na Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Bi. Erin Browne, pamoja na viongozi na maafisa mbalimbali kutoka nchi shiriki.

About the author

Alex Sonna