Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi, Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Puma Enegy Tanzania, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kampuni hiyo, Bi. Fatma Abdallah, wakati wa kikao kilichojadili maeneo ya kimkakati, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi, Khamis Mussa Omar (Mb), akiongoza kikao chake na Ujumbe wa Kampuni ya Puma Enegy Tanzania, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bi. Fatma Abdallah, wakati wa kikao kilichojadili maeneo ya kimkakati, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Puma energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Fedha kilicholenga kujadili maeneo ya kimkakati, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akifafanua jambo katika kikao cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi, Khamis Mussa Omar (Mb), na Ujumbe wa Puma Enegy Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kampuni hiyo Bi. Fatma Abdallah, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Ujumbe wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Puma energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Fedha, katika kikao kilicholenga kujadili maeneo ya kimkakati, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi, Khamis Mussa Omar (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Puma energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah,baada ya kikao chao kilichojadili maeneo ya kimkakati, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Ujumbe wa Wizara ya Fedha ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi, Khamis Mussa Omar (Mb), ukiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bi. Fatma Abdallah, baada ya kikao chao kilichojadili maeneo ya kimkakati, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma.)
Na Peter Haule na Saidina Msangi, WF, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameipongeza Kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa jitihada zake za kuongeza uwekezaji na kuboresha uendeshaji wa kampuni, hatua iliyowezesha Serikali kupata gawio la Sh. bilioni 15.
Mhe. Balozi Omar alitoa pongezi hizo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Puma Energy Tanzania, ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bi. Fatma Abdallah, katika Ofisi za Wizara ya Fedha Treasury Square.
“Utoaji wa gawio ni ishara kwamba kampuni inaendelea kufanya vizuri na kupata faida, jambo ambalo pia linaongeza mchango wake katika maendeleo ya nchi,” alisema Mhe. Balozi Omar.
Mhe. Balozi Omar alieleza kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha sekta ya nishati inaendelea kuwa imara na kufanya vizuri, licha ya changamoto zinazojitokeza katika soko la nishati duniani.
Alisema hatua hizo zinalenga kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za nishati kwa gharama nafuu na kupunguza athari za mabadiliko ya bei za nishati.
Aidha, alisema Serikali itaendelea kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa haki katika sekta ya nishati ili kulinda maslahi ya wananchi, wakati huo huo kuhakikisha mapato ya Serikali hayaathiriki na ushindani usio na tija.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, aliipongeza Serikali kwa jitihada inazochukua katika kuhakikisha sekta ya nishati inaendelea kuwa imara na wananchi wanapata huduma stahiki.
Alisema Puma Energy Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali na kuimarisha shughuli zake ili kuongeza mchango wake kwa Taifa, ikiwemo kuongeza gawio kwa Serikali.
Bi. Abdallah pia alisema jitihada zinazofanywa na Serikali zimechangia kushuka kwa gharama za mafuta, jambo ambalo linaendelea kuwa na manufaa kwa wananchi na uchumi kwa ujumla.