Na Mwandishi Wetu-LONDON, UINGEREZA –

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameshiriki Mkutano Mkuu wa Afrika ulioandaliwa na African Leadership Magazine kwa kushirikiana na African Leadership Organization (ALO), unaofanyika jijini London, Uingereza.

Mkutano huo umewakutanisha viongozi wa serikali, sekta binafsi, taasisi za maendeleo, wasomi na wadau mbalimbali kutoka Afrika na sehemu nyingine za dunia kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya bara hilo.

Majadiliano yamejikita katika masuala ya uongozi, uwekezaji, biashara na ushindani wa kiuchumi, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo, “From Vision to Velocity: Driving Africa’s Next Wave of Growth & Leadership.”

Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Dkt. Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ya African Leadership Organization (ALO), aliongoza kikao cha bodi hiyo kilichojadili mikakati ya kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi barani Afrika.

Kikao hicho kilijadili pia namna ya kuimarisha uongozi bora, kuvutia uwekezaji na kuongeza ushirikiano wa kimataifa ili kuchochea maendeleo endelevu ya bara la Afrika.

Bodi ya Washauri ya ALO inajumuisha viongozi na wataalamu mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali duniani. Miongoni mwa wajumbe wake ni Makamu wa Rais Mstaafu wa Liberia, Jewel Howard Taylor; Mkurugenzi wa Adam Global Holdings, Tahir Akhtar; Victor Oladokun wa African Development Bank; Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Africa Ventures Advisory nchini Ujerumani, Christian Lindfeld; Kamanda Mkuu Mstaafu wa Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika (AFRICOM), J