Featured Kitaifa

MATENDO YA HURUMA

Written by Alex Sonna

Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Ikungi Mashariki Miraji Mtaturu, amefika Hospitali ya Wilaya Ikungi kumjulia hali mke wa Katibu wake Ally Juma Rehani ambaye amelazwa hapo akiendelea kupatiwa matibabu.

Mtaturu ametumia nafasi hiyo kumtakia uponyaji wa mapema ili arejee kwa majukumu yake ya kuihudumia familia yake.

Mtaturu ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ambayo kwa sasa inatoa huduma zote ikiwemo upasuaji mkubwa na mdogo hivyo kuboresha huduma za afya kwa wananchi wetu.

Amewatakia wananchi wote wa Ikungi na Tanzania kwa ujumla Sikukuu njema ya Pasaka.

About the author

Alex Sonna