Featured Michezo

REFA ASHUSHWA DARAJA KISA DIARRA,MSAIDIZI WAKE AFUNGIWA KISA MWANENGO

Written by Alex Sonna

MWAMUZI wa Mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar ,Gilbert Mrina kutoka Kilimanjaro ameshushwa daraja kwa kosa la kushindwa kumchukulia hatua Djigui Diarra kwa utovu wa nidhamu alioonyesha katika mchezo huo.

Mwamuzi Msaidizi Abdulaziz Ally kutoka Arusha,amefungiwa mizunguko mitano kwa kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu kwenye mchezo huo baada ya kunyoosha kibendera juu kuashiria mshambuliaji wa Yanga SC,Emmanuel Mwanengo aliotea.

Tukio hilo lilitokea katika dakika ya 36 ya mchezo huo ambapo kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya TPLB imesema hakukuwa na kosa la kuotea kwa mujibu wa sheria za mpira wa miguu kwani Mwanango hakuwa kwenye eneo la kuotea kabla ya kupokea pasi kutoka kwa Pacome Zouzoua

About the author

Alex Sonna