Featured Kitaifa

SIKU 100 ZA SAMIA: WAZIRI GWAJIMA ATAJA MAFANIKIO LUKUKI YA WIZARA YAKE

Written by Alex Sonna

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 25,2026 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma kuhusu mafanikio makubwa ya siku 100 katika sekta ya Viwanda na Biashara baada ya uchaguzi Mkuu.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 25,2026 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma kuhusu mafanikio makubwa ya siku 100 katika sekta ya Viwanda na Biashara baada ya uchaguzi Mkuu.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa ndani ya siku 100 tangu kuapishwa kwa Awamu ya Pili ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,Wizara hiyo  mafanikio makubwa yanayopimika na yenye kugusa moja kwa moja maisha ya wananchi katika utambuzi, urasimishaji na uwezeshaji wa wafanyabiashara ndogondogo na wajasiriamali katika sekta isiyo rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari Januari 25, 2026 jijini Dodoma, Waziri Dkt.Gwajima amesema jumla ya WBN 119,595 wamepata usajili rasmi kupitia Mfumo wa Usimamizi na Usajili wa Wafanyabiashara Ndogondogo (WBN–MIS), ikiwemo wanawake 73,341 na wanaume 46,254. Miongoni mwao, Machinga 103,102, Mama na Baba Lishe 12,384, na waendesha bodaboda na bajaji 4,109.

Aidha, wizara imetoa Shilingi 10.5 bilioni kwa ajili ya mikopo yenye riba ya asilimia 7 kwa wafanyabiashara ndogondogo, ambapo tayari Shilingi 1.35 bilioni zimekwishatolewa kwa wafanyabiashara 588 kupitia Benki ya NMB. Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, Shilingi 337.97 milioni zimetolewa kwa wanawake wajasiriamali 45 kwa riba ya 4%.

“Kupitia TRA, waendesha bodaboda na bajaji 209,632 wamepata leseni za udereva, na kupitia mfumo wa Wezesha Portal, jumla ya vikundi 6,041 vimepatiwa usajili na kufanikishwa kupata mikopo, ikiwemo vikundi vya wanawake 3,207, vijana 2,318 na watu wenye ulemavu 516, vikijumuisha wajasiriamali 30,205.”amesema Dkt.Gwajima

Hata hivyo Dkt.Gwajima amesema  kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kwa ushirikiano na SIDO, wajasiriamali 16,325 wamepata urasimishaji, 11,000 wameruhusiwa mafunzo ya ujasiriamali, na zaidi ya 3,900 wamenufaika na namba za mlipa kodi (TIN) na leseni za biashara. Pia, mikopo 265 yenye thamani ya Shilingi 1.08 bilioni imetoa ajira 652, ambapo ajira za vijana ni 489.

Amesema kuwa Sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na madini zimepata usajili na uwezeshaji wa wajasiriamali na wafanyabiashara ndogondogo, ikiwemo wakulima 532,023, wavuvi 2,100, wafugaji viumbe maji 2,478, na wachimbaji wadogo wa madini 2,239. Jumla ya Shilingi 33.45 bilioni zimepatiwa vikundi mbalimbali vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mfumo wa Halmashauri.

” Serikali imeongeza huduma karibu na wananchi kupitia midahalo ya makundi rika 9,545, mfumo wa mawasiliano mtandaoni www.nis.jamii.go.tz, na kituo cha huduma kwa wateja ambacho kimepokea changamoto 425,075. Sekretarieti ya Jukwaa la Kitaifa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi imezinduliwa kuhakikisha wanawake wanapata fursa za kiuchumi kutoka sekta zote.”amesema

Aidha Dkt.Gwajima amesema kuwa huduma za ustawi wa jamii pia zimeimarishwa, ikiwemo walengwa 171,529 kuhusiana na Wazee, watoto, wenye ulemavu na manusura wa ukatili, huku watoto 2,699 wameunganishwa na familia zao. Vilevile, madawati 2,479 katika vituo vya usafirishaji yamehudumia watu wazima.

Amesema kuwa Serikali pia imetekeleza urasimishaji wa vikundi 1,216 katika ununuzi wa umma (NeST), ambapo vikundi 1,123 vimepata zabuni, ikiwemo wanawake 426, vijana 630, watu wenye ulemavu 25, na wazee 42, ikiwapa fursa ya kushiriki asilimia 30 ya manunuzi ya umma.

 “Mafanikio haya ni misingi ya uchumi jumuishi, shindani na endelevu, na serikali itaendelea kushirikiana na wizara, taasisi, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha hakuna Mtanzania anayebaki nyuma.”amesema Dkt. Gwajima

Dkt. Gwajima ameongeza kuwa wananchi wanaweza kupata huduma na taarifa kupitia call centre ya wizara kwa namba 0766400168, 0734986503, 0769608130, 0262160250, WhatsApp 0774112233, au kwa masuala ya watoto piga 116.

About the author

Alex Sonna