Featured Kitaifa

SIKU 100 ZA SAMIA: WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAANIKA MAFANIKIO 12 MAKUBWA

Written by Alex Sonna

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24,2026 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma kuhusu mafanikio makubwa ya siku 100 katika sekta ya Viwanda na Biashara baada ya uchaguzi Mkuu.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga,akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari leo Januari 24,2026 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma kuhusu mafanikio makubwa ya siku 100 katika sekta ya Viwanda na Biashara baada ya uchaguzi Mkuu.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24,2026 katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma kuhusu mafanikio makubwa ya siku 100 katika sekta ya Viwanda na Biashara baada ya uchaguzi Mkuu.

Msemaji Mkuu wa Serikali na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.Gerson Msigwa,akizungumza na waandishi wa habari wakati Wizara ya Viwanda na Biashara ikiwasilisha  mafanikio makubwa ya siku 100 katika sekta ya Viwanda na Biashara baada ya uchaguzi Mkuu.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema kuwa ndani ya siku 100 tangu kuapishwa kwa Awamu ya Pili ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya viwanda na biashara imepata mafanikio 12 yanayopimika na yenye kugusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Januari 24, 2026 jijini Dodoma, Waziri Kapinga amesema mafanikio hayo yametokana na utekelezaji thabiti wa ahadi za Rais Samia za kujenga uchumi wa viwanda unaozalisha ajira, kukuza kipato cha wananchi na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara kikanda na kimataifa.

UWEZESHAJI WA WAJASIRIAMALI NA AJIRA

Amesema Serikali imefanikiwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia utoaji wa mikopo 193 yenye thamani ya Shilingi milioni 821.7, pamoja na kuchochea uongezaji thamani wa mazao ya kilimo kupitia viwanda vidogo na vya kati.

“Mikopo hiyo imetolewa kupitia Mfuko wa National Entrepreneurship Development Fund (NEDF) na Credit Guarantee Scheme (CGS) katika mikoa 19 ikiwemo Tanga, Tabora, Katavi, Pwani, Rukwa, Iringa, Morogoro, Ruvuma, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Songwe, Shinyanga, Dodoma, Singida, Manyara, Kagera na Kigoma,” amesema Waziri Kapinga.

Ameeleza kuwa mikopo hiyo imezalisha jumla ya ajira 546 katika sekta za viwanda, ufugaji, kilimo, biashara na huduma, ambapo ajira 436 ni kwa vijana.

KONGANI NA MITAA YA VIWANDA

Kuhusu maendeleo ya kongani na mitaa ya viwanda, Waziri Kapinga amesema mikoa 11 imekamilisha miradi hiyo, huku maeneo manne yakiwa tayari kwa uzinduzi rasmi Februari 2026.

Maeneo hayo ni pamoja na:SIDO Kigoma yenye viwanda 46 vitakavyotoa ajira 205 (vijana 75),
SIDO Morogoro yenye viwanda 8 vinavyotoa ajira 32 (vijana 22),
SIDO Mbeya yenye viwanda 65 vya mafuta ya alizeti na mpunga vinavyotoa ajira 4,330 (vijana 844),
SIDO Singida yenye viwanda 8 vinavyotoa ajira 52 (vijana 36).

UWEKEZSJI VIWANDA VIKUBWA

Katika uwekezaji wa viwanda vikubwa, Waziri Kapinga amesema kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Serikali imefanikiwa kuvutia wawekezaji watatu wakubwa katika Kongani ya Viwanda ya TAMCO, hali inayoonesha kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji nchini.

Wawekezaji hao ni: Hyundai Automobile Manufacturing, anayejiandaa kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari katika eneo la mita za mraba 88,799;
Goodlife Investment Tanzania, anayetarajiwa kuanza uunganishaji wa magari ya umeme (Electric Vehicles) katika eneo la mita za mraba 17,460;Sanda Max Group Limited, anayejenga kiwanda cha kuzalisha chakula cha mifugo katika eneo la mita za mraba 17,390.

Amesema viwanda hivyo vinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 150 na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 500.

URASIMISHAJI WA BIASHARA NA UBUNIFU
Kwa upande wa urasimishaji wa biashara na ulinzi wa ubunifu, Waziri Kapinga amesema Wizara kupitia BRELA imeongeza kasi ya huduma hizo ambapo ndani ya siku 100: Kampuni 4,233 zimesajiliwa, kati ya hizo 2,915 ni za vijana; Majina ya biashara 7,498 yamesajiliwa, ambapo 4,742 ni ya vijana; Alama za Biashara na Huduma 881 zimesajiliwa; Leseni za Viwanda 141 zimetolewa, kati ya hizo 129 ni za vijana;
Leseni za Biashara Kundi “A” 4,907 zimetolewa.

MAZAO YA KIMKAKATI

Amesema katika sekta ya mazao ya kimkakati, zaidi ya Shilingi trilioni moja zimelipwa kwa wakulima wa korosho kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala, huku tafiti za madini adimu na kimkakati zikianza rasmi katika mikoa ya Kagera na Singida.

Kwa  wake Msemaji Mkuu wa Serikali na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.Gerson Msigwa,amewasihi watanzania kutumia taarifa rasmi zinazotolewa na serikali kutoka kwenye vyanzo sahihi,ikiwemo tovuti ya serikali.

About the author

Alex Sonna