CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)kimepeleka tabasamu kwa watoto wanaolelewa Kituo cha kulea watoto wanaishi katika mazingira magumu cha Malaika Kids kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kuwapatia vyakula ,vinywaji pamoja na vifaa vya shule kwa watoto wa kituo hicho.
Akizungumza leo Desemba 20,2025 wakati akikabidhi vyakula,vinywaji na vifaa vya shule,Katibu wa NEC mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa(SUKI) Rabia Abdalla Hamid amesema katika kuelekea katika sikukuu za mwisho wa mwaka Chama Cha Mapinduzi kimeona haja ya kuwapa tasabamu watoto wa Taifa la Tanzania na wameanza na Kituo cha Malaika Kids cha jijini Dar es Salaam.
“Nimetumwa na Chama changu kuleta tabasamu katika kituo hiki cha kulea watoto cha Malaika Kids na mimi kama mkuu wa idara wa mambo ya siasa na uhusiano wa kimataifa ambae pia ninaesimamia na kufatilia maendeleo ya jumuiya za kijamii nimeelekezwa nije kukabidhi zawadi kwa ajili ya watoto wetu hasa wanaoishi katika mazingira magumu
“Tunafahamu Rais wetu mpendwa Dk.Samia Suluhu Hassan aliahidi kuacha tabasamu , hivyo sisi wasaidizi wake tumeamua kufikisha tabasamu kwa watoto hawa.Pia niwahakikishie CCM itaendelea kuyafikia makundi yote katika jamii ya Watanzania.”
Rabia Abdalla Hamid amesisitiza pamoja na kukabidhi zawadi hizo pia ujumbe wao mkubwa kwa watoto hao watambue wao wapo na viongozi wa taifa hili wanatambua uwepo wao.
Kwa upande wake Mwanzilishi Mwenza wa Kituo cha Malaika Kids Charles Nyimbo amekishukuru Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka watoto wa kituo hicho na kwamba watoto wa kituo hicho wanatambua upendo alionao Rais Samia kwa watoto wa Taifa hili.
Katibu wa NEC mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa(SUKI) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rabia Abdallah Hamid(kushoto)akimkabidhi kompasi mmoja ya watoto wanaolelewa katika Kituo cha Malaika Kida kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwanzilishi Mwenza wa kituo hicho Charles Nyembo na wa pili kushoto ni Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake(UWT) Wilaya ya Kinondoni
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

