Featured Kitaifa

WATANZANIA 8 WAVUNA MILIONI 12, DROO YA PILI YA ‘MAGIFTI YA MIXX PESA’

Written by Alex Sonna

 

Na Mwandishi wetu -Dar es salaam  

Watanzania wanane kutoka mikoa mbalimbali wamekabidhiwa jumla ya shilingi milioni 12 kupitia droo ya pili ya kampeni ya ‘Magifti ya Mixx Pesa’ iliyoandaliwa na kampuni ya huduma za kifedha kidijitali, Mixx.

Hafla ya kukabidhi zawadi hizo imefanyika jijini Dar es Salaam, ikiwahusisha washindi kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Geita na Morogoro, huku kila mshindi akinufaika kwa kiasi kilichochochea furaha na matumaini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Wateja Maalum wa Mixx, Bi. Marry Ruta, alisema kampeni hiyo inalenga kuwashukuru wateja kwa uaminifu wao na kuwagusa kiuchumi katika kipindi cha mwisho wa mwaka.

Alibainisha kuwa washindi wamepatikana kutokana na matumizi ya mara kwa mara ya huduma za Mixx ikiwemo kuweka pesa, Lipa kwa Simu, kununua vifurushi pamoja na mikopo ya Nivushe Plus na Bustisha.

Bi. Ruta aliwahimiza wateja kuendelea kufanya miamala ili kuongeza nafasi ya kushinda katika droo zijazo kabla ya kampeni hiyo kufikia tamati.

Miongoni mwa washindi ni Bw. Anuary Mwinyi, dereva na mkazi wa Bunju, aliyesema ushindi huo umefika wakati muafaka kwake katika kukabiliana na changamoto za maisha.

Alisema fedha hizo atazitumia kuendeleza biashara zake, kushughulikia mahitaji ya familia na pia kumsaidia mke wake katika shughuli za kila siku.

                         Washindi  kutoka mikoa mbalimbali  wa ‘Magifti ya Mixx Pesa

Kwa upande wao, washindi wengine waliishukuru Mixx kwa fursa hiyo, wakisema kampeni ya ‘Magifti ya Mixx Pesa’ iliyoanza Desemba 2, 2025 na kumalizika Januari 4, 2026, imeleta faraja kubwa katika msimu wa sikukuu.


 

 

About the author

Alex Sonna