Featured Kitaifa

USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA NI NGUZO YA KUKUZA UCHUMI WA WANANCHI- BI. CONSOLATA

Written by mzalendo
Na Mwandishi Wetu- Dodoma 

Shirikisho la Vyama Vya Ushirika (TFC) limefanya Mkutano wa Viongozi wa Jukwaa la Wanawake wa Ushirika Tanzania Bara umefunguliwa rasmi leo Desemba 19,2025 jijini Dodoma, ukiwakutanisha viongozi Wanawake wa Jukwaa la Ushirika kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kujadili nafasi ya mwanamke katika Ushirika na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Naibu Mrajisi uhamasishaji kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bi. Consolata Kiluma, amesema kuwa ushiriki wa wanawake katika vyama vya ushirika ni nguzo muhimu ya kukuza uchumi wa wananchi.

Aidha, amesema pamoja na mkutano huo kuwa sehemu ya uandaaji wa Katiba ya jukwaa hilo wanapaswa kuweka viashiria vya utendaji kazi vya kupima (KPI) utekelezaji wa mikakati wanayokubaliana pale wanapokutana kwenye vikao. 

“Hicho ndo kitu ambacho nasisitiza pamoja na kazi kubwa Mtakayoifanya Siku ni pamoja na hayo tunataka jukwaa letu la wanawake liwe kuwa lenye kuleta tija hii itasaidia katika kuonesha kile ambacho tunakifanya na kinaoneka,”amesema. 

Mkutano huo umeelezwa kuwa jukwaa la kujadili changamoto zinazowakabili wanawake Fursa zilipo katika vyama vya ushirika, ikiwemo upatikanaji wa mitaji, uongozi na masoko, pamoja na kutafuta suluhisho litakalowawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.

Kwa upande Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC), Bw. Fares Muganda amesema ikiwa watatumia vyema jukwaa hilo ndani ya ushirika wanawake wengi wataona faida ya kujiunga na ushirika, jambo litakalosaidia kujenga nguvu ya pamoja itakayowasaidia kuweza kufanya shughuli za kiuchumi. 

“Niwaahidi kuwa sisi kama TFC tutakuwa pamoja katika kuhakikisha kwamba jukwaa hili linaleta mafanikio makubwa kwa wanawake washirika Tanzania, “amesema. 

Naye Mwenyekiti jukwaa hilo la Wanawake Bi. Pili Marwa amesema katika kubaliana na changamoto ya kutokumbulika kwa jukwaa hilo watahakikisha kupitia mkutano huo wanaandaa nyaraka zote ikiwemo Katiba na miongozo mbalimbali itakayosaidia kutambulika kitaifa na kimataifa.

Ushirika Pamoja Tuujenge Uchumi!

 

 

About the author

mzalendo