Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza Kikao Kazi kilichowajumuisha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, kilichofanyika leo tarehe 24 Novemba 2025 Ikulu. Kikao Kazi hicho ni cha kwanza tangu Kipindi cha Pili cha Serikali ya Awamu ya Nane kuingia madarakani.
