Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25 uliomalizika leo Oktoba 24,2025 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna, Dodoma
SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa elimu inaendelea kutekeleza mikakati kabambe ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, ili kuhakikisha sekta hiyo inazidi kuboreshwa na kuwa jumuishi zaidi.
Akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25 leo Oktoba 24,2025 jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo, amesema serikali inajivunia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika sekta hiyo na imejipanga kuongeza fursa za elimu kwa Watanzania.
“Tutaimarisha na kuongeza matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji, sambamba na kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali muhimu kwa ajili ya elimu,” amesema Prof. Nombo.
Aidha, amebainisha kuwa serikali imeweka mpango mahsusi wa kuongeza idadi ya walimu wa masomo ya sayansi, biashara na ufundi, ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira na mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea nchini.
Prof.Nombo amesema kuwa wataendelea kuiboresha sekta ya elimu nchini, ikiwemo kuimarisha maslahi ya walimu ili waweze kufundisha kwa weledi na kutoa elimu bora kwa vijana.
Hata hivyo Prof.Nombo, amesema walimu wana jukumu kubwa la kuhakikisha elimu ya Tanzania inakuwa ya tija, inayowawezesha vijana kujiajiri au kuajiriwa kulingana na mazingira wanayokabiliana nayo.
“Ni muhimu kuimarisha walimu wa sayansi, ufundi na biashara pamoja na kurahisisha upatikanaji wa rasilimali za ufundishaji ili elimu yetu iingie katika soko shindani la ajira,” amesema Prof.Nombo.
Prof. Nombo amewashukuru wadau wote wa elimu kwa ushirikiano wanaoutoa katika kuboresha sekta hiyo na kupongeza walimu kwa mchango wao mkubwa katika kuelimisha taifa.
“Hakuna elimu bila mwalimu, kwani ndio msingi wa kujenga nguvu kazi ya Tanzania yenye maarifa na ujuzi, tayari kushindana katika soko la ajira kitaifa na kimataifa,” ameeleza Prof. Nombo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Elimu), Bw. Atupele Mwambene, amesema ili kufanikisha lengo la serikali la kupata vijana wenye uwezo mkubwa watakaoingia katika soko shindani la ajira, ni lazima kuimarishwa elimu ya awali na sekondari, ambayo ndiyo msingi wa kuwajenga vijana hao.
“Sisi kama sekta ya elimu bado tuna fursa za kufanya vizuri zaidi, kwa kuboresha na kuimarisha utendaji katika elimu ya awali, msingi na sekondari ili kuongeza upatikanaji wa elimu kwa vitendo,” amesema Mwambene.
Dk. John Lusingu, mmoja wa wadau wa elimu kutoka Development Partners (DPs), amesema wadau wataendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha juhudi za kuboresha elimu nchini zinafanikiwa.
Mkutano huo umehudhuriwa na washiriki 367, wakiwemo wadau wa maendeleo, sekta binafsi, FBOs, taasisi za elimu ya juu, na walimu wa shule za msingi na sekondari, ambao wameshiriki kikamilifu katika mjadala na tathmini za utekelezaji wa sera ya elimu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25 uliomalizika leo Oktoba 24,2025 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25 uliomalizika leo Oktoba 24,2025 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Elimu), Bw. Atupele Mwambene,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25 uliomalizika leo Oktoba 24,2025 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo- (hayupo pichani) wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25 uliomalizika leo Oktoba 24,2025 jijini Dodoma.

Wadau wa Elimu pamoja na wanafunzi wakichangia mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25 uliomalizika leo Oktoba 24,2025 jijini Dodoma.