Featured Kitaifa

DAKIKA ZA LALA SALAMA,DKT NCHIMBI ATUA KILWA KUSAKA KURA ZA USHINDI WA CCM.

Written by Alex Sonna

Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi mapema leo Oktoba 20, 2025 amewasili katika uwanja wa ndege wa Kilwa mkoani Lindi,ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya Kampeni ya kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Ikiwa zimebaki siku 9 za lala salama kufikia uchaguzi mkuu,Dkt. Nchimbi anatarajia kufanya mkutano wake wa hadhara wa kampeni wa kunadi Sera na Ilani ya CCM (2025-2030) katika kata ya Tingi, jimbo la Kilwa Kaskazini na kuomba ridhaa ya wananchi kukipigia kura za ndio chama hicho kupitia wagombea wake katika nafasi zote kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.

About the author

Alex Sonna