Featured Kitaifa

WAKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO WAFANYA MAPITIO YA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA

Written by Alex Sonna

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha, Bw. Moses Tesha, akifungua Kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta chenye lengo la kujadiliana na kupanga mipango kwa pamoja, Kikao kazi kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

Na. Peter Haule, WF, Arusha

Serikali kupitia Wizara ya Fedha, imefanya kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta, ikiwa ni sehemu ya mchakato endelevu wa kuboresha utekelezaji wa bajeti na kuhakikisha uwazi, tija na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma.

Akifungua kikao kazi hicho, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha Bw. Moses Tesha, alisema kuwa Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review- PER) ni takwa la kisheria chini ya Sheria ya Bajeti Sura ya 439 na Kanuni zake, na hufanyika kila mwaka wa fedha.

Alifafanua kuwa Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma (PER) kwa mwaka wa fedha 2024/25 yanalenga kupitia mwenendo wa matumizi katika sekta muhimu za maendeleo ambazo ni Afya, Elimu, Maji na Kilimo, kwa lengo la kuboresha maandalizi ya bajeti ya mwaka 2026/2027.

Bw. Tesha, alisema kuwa Serikali inalenga kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa, na kwa namna inayokuza uchumi na kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma siyo jambo jipya, bali ni utaratibu ambao umefanyika kwa miaka mingi hadi mwaka 2016 kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo, kuanzia mwaka wa fedha 2023/24 Serikali iliamua kuhuisha mchakato huo kwa kuhusisha zaidi taasisi za ndani na wadau wa ndani wa maendeleo, ili kuongeza umiliki na usimamizi wa ndani wa fedha za umma”. Alisema Bw. Tesha.

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, alisema ili Serikali iweze kufikia malengo ya utekelezaji wa Bajeti katika kukuza uchumi na kutoa huduma kwa wananchi, inahitaji muda wa kujiuliza na kujitathmini, jambo ambalo Wizara ya Fedha imeamua kuratibu na kutekeleza jambo hilo kupitia Kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, ngazi ya sekta

Bw. Anyingisye alisema kuwa umuhimu wa Kikao kazi hicho ni kuisaidia Serikali kutekeleza na kupanga mipango kwa pamoja hivyo Kikao hicho ni fursa ya pekee kama Serikali kuangalia imetoka wapi, ipo wapi na nini kinatakiwa kifanyike ili kuboresha.

Alisema katika kufanikisha jambo hilo Kikao kinawashirikisha wadau kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu ambao ni think tank wanao itazama Serikali kwa jicho tofauti hivyo kuweza kubainisha maeneo ya kuboresha, lakini pia inashirikisha Taasis zisizo za Serikali na taasisi za utafiti.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Chuo Kikuu cha Dodoma, Dkt. Evodius Kanyamyoga, alisema vikao hivyo ni mwendelezo wa Kikao kilichofanyika mwaka uliopita ambacho kinamanufaa makubwa katika Sekta za maendeleo zikiwemo za Serikali na Binafsi.

Alisema kuwa wamewasikiliza wadau mbalimbali katika ngazi ya Kitaifa hadi Halmashauri ambao wamebainisha maeneo yanayopaswa kuboreshwa ili kuleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla na mambo hayo yana nafasi kubwa ya kuboreshwa katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Kikao hicho, kimewashirikisha Wakurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara zote za Kisekta, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Asasi zisizo za kiserikali na Wizara ya Fedha.

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha Bw. Meshack Anyingisye (kulia), Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha, Bw. Moses Tesha, wakiwasili katika ukumbi wa Simba,  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha, kushiriki Kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta.

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha, Bw. Moses Tesha, akifungua Kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta chenye lengo la kujadiliana na kupanga mipango kwa pamoja, Kikao kazi kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha Bw. Meshack Anyingisye akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta ambapo alisema Kikao hicho kinaunganisha mawazo kutoka sekta mbalimbali za Serikali na Binafsi ili kuwa na mipango yenye tija, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Fundi Makama, akiwataka wajumbe wa  kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta, kushiriki kikamilifu katika Kikao kazi hicho ili kuleta tija,  kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

Afisa wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Amede Andrea, akieleza utaratibu wa Kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bw. Sigsbert Kavishe akitoa mada kuhusu malengo ya Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER), wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha Bw. Meshack Anyingisye (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Julieth Magambo, wakati wa Kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha

 

Wakurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali pamoja na wadau wengine wakiwa kwenye Kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

Meza kuu ikiongozwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha, Bw. Moses Tesha, (katikati), Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha Bw. Meshack Anyingisye (wa pili kushoto), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha Bw. Fundi Makama (kushoto)kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Bw. Sigsbert Kavishe, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Nishati, Bw. Petro Lyatuu, Wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha Public Expenditure Review -PER, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

Meza kuu ikiongozwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Arusha, Bw. Moses Tesha, (katikati), Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha Bw. Meshack Anyingisye (wa pili kushoto), Wakiwa katika picha ya pamoja Wakurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara na Taasisi  mbalimbali wakati wa Kikao kazi cha Mapitio ya Matumizi ya Fedha za Umma, (Public Expenditure Review -PER) ngazi ya sekta, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) mkoani Arusha.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Fedha, Arusha)

About the author

Alex Sonna