Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi waliofika kumsikiliza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mama Salmini, Mlandizi ndani ya jimbo la Kibaha Vijijini leo Ijumaa Oktoba 10, 2025 mkoani Pwani.
Katika mkutano huo, Dkt.Nchimbi pamoja na kunadi Sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030,pia alimuombea kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani.
Pamoja na mambo mengine,Dkt Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha Mjini Ndugu Silyvestry Francis KOKA, mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Ndugu Hamoud Abuu Jumaa pamoja na Madiwani.