Featured Kitaifa

GNRC WAONGEZA UELEWA KWA BODABODA MTWARA ‘KUJENGA AMANI’ KIPINDI CHA UCHAGUZI

Written by Alex Sonna
Shirika lisilo la kiserikali la GNRC limeendeleza kampeni ya “Kujenga Amani” kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Safari Media Mtwara, Tasa Tanzania na Malunde Media.
 
Lengo kuu la kampeni hii ni kuwahimiza vijana, hususan maafisa usafirishaji (bodaboda) waliopo mkoani Mtwara, kufanya maamuzi sahihi katika utekelezaji wa shughuli zao ili kuchangia katika kuimarisha amani na si kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.
Afisa miradi kutoka Shirika la Tasa Tanzania, Betty Chenge amesema kuwa vijana wana nafasi ya kipekee katika kujenga au kubomoa amani.
“Vijana wanapotumika vizuri, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi, watakuwa nguzo muhimu ya maendeleo kwa jamii zao,” amesema Chenge.
Kampeni hii inasisitiza kuwa vijana ni wadau muhimu wa maendeleo, na kuwa na uwajibikaji katika jamii kunasaidia kutengeneza mazingira ya amani, uthabiti, na maendeleo endelevu.

About the author

Alex Sonna