Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara nchini Tanzania Dkt. Hashil Abdallah na Katibu Mkuu Idara ya Biashara, Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Kenya wakisaini hati ya makubaliano wakati wa Mkutano wa Tisa (9) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya unaofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Dar es Salaam nchini Tanzania Oktoba 01, 2025.
……
Tanzania na Kenya zimeondoa vikwazo vya biashara visivyo vya kiushuru vinne (4) kati ya 14 vilivyojadiliwa katika Mkutano wa Tisa (9) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya nchi hizo ambapo hatua hii inatimiza vikwazo 58 vilivyotatuliwa kati ya 68 vilivyokuwepo huku vikwazo 10 vilivyobakia kutatuliwa ifikapo Machi 31, 2026
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah Oktoba 1, 2025 wakati wa Mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam ambapo nchi hizo mbili zilijadili vikwazo hivyo na kutia saini makubaliano hayo ili kutumiza maelekezo ya makubaliano yaliyowekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya, Mhe Dkt. William Ruto, wakati wa Ziara nchini Tanzania Oktoba 9–10, 2022 kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa Biashara’s baina ya Nchi hizo.
Aidha Dkt Abdallah amebainisha vikwazo vilivyoondolewa vikijumuisha kuondoa kodi ya zuio kwa bia za TBL kwenda Kenya, Mihuri ya ushuru (Tax Stamps Pamoja na Ada na Tarantino usafirishaji wa Bidhaa za mifugo kutoka Kenya kutekelezwa kwa kufuata maamuzi ya Baraza la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya yaAfrika Mashariki (EAC) na kuondoa Bima ya COMESA kwa kuwa haihusiani na Tanzania
Vilevile, amesema Nchi hizo zimeahidi kushirikiana katika kuhakikisha biashara kati ya Tanzania na Kenya inafanyika kwa haki, kwa kuzingatia mikataba ya EAC na kuwasilisha masuala mapya kupitia njianza idiomatic ndani ya Mwezi mmoja baada ya Mkutano huo.
“Tumekubaliana kwamba ndani ya miezi sita, ifikapo Machi 31, vikwazo vyote vitakuwa vimekwisha na suluhu zao zitatolewa kikamilifu. Kila sekta na idara ina jukumu la kukutana na upande wa pili, kujadiliana kwa pamoja na kutafuta njia za kudumu za kuyatatua. Wataalamu pia wanashirikiana kwa karibu kusaidia wafanyabiashara kuhakikisha biashara inafanyika kwa urahisi na ufanisi.
Kwa upande wa Kenya, Katibu Mkuu wa Biashara katika Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Bi Regina Ambam, alieleza kuwa makubaliano hayo ni hatua muhimu katika kurahisisha mifumo na kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki na ustawi wa wananchi kwa ujumla huku
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kujiandaa kwa biashara ya kidijitali na ni hatua ya kihistoria katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kuchochea ujumuishaji wa kikanda na kuiweka Afrika Mashariki katika nafasi ya ushindani duniani,”
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kenya Bi Carolyne Karugu amesema Kamati Hiyo ya Pamoja imefanikiwa kuondoa vikwazo hivyo vya biashara visivyo vya kiushuru kwa asilimia 78. yanatokana na makubaliano yaliyowekwa wakati wa ziara rasmi ya Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto, nchini Tanzania Oktoba 9–10, 2022
Kwa ajili ya ustawi wa Jumuiya nzima ya Afrika Mashariki.” hatua inayoimarisha uhusiano ya nchi mbili na kuleta athari chanya za kiuchumi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara nchini Tanzania Dkt. Hashil Abdallah na Katibu Mkuu Idara ya Biashara, Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Kenya wakisaini hati ya makubaliano wakati wa Mkutano wa Tisa (9) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya unaofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Dar es Salaam nchini Tanzania Oktoba 01, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara nchini Tanzania Dkt. Hashil Abdallah na Katibu Mkuu Idara ya Biashara, Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Kenya wakibadilishana hati ya makubaliano wakati wa Mkutano wa Tisa (9) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya unaofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Dar es Salaam nchini Tanzania Oktoba 01, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara nchini Tanzania Dkt. Hashil Abdallah na Katibu Mkuu Idara ya Biashara, Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Kenya wakionyesha hati ya makubaliano wakati wa Mkutano wa Tisa (9) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya unaofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Dar es Salaam nchini Tanzania Oktoba 01, 2025.