Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, akizungumza wakati wa ziara yake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 29 Septemba, 2025.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, akisalimiana na Wazee wakati wa ziara yake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 29 Septemba, 2025.
Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida Lusajo Kafuko akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju katika Makazi hayo tarehe 29 Septemba, 2025.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, akitoa zawadi ya mbuzi na vyakula kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ziara yake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 29 Septemba, 2025.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, akitoa zawadi ya televisheni kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ziara yake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 29 Septemba, 2025.
Wazee wanaolelewa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amoni Mpanju wakati wa ziara yake katika Makazi hayo tarehe 29 Septemba, 2025. (Picha zote na Jackline Minja WMJWM)
Na Jackline Minja WMJJWM, Manyoni, Singida.
Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kudumisha huduma bora kwa wazee kwa kuhakikisha kundi hilo linapata huduma za msingi zinazowawezesha kuishi maisha yenye heshima na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
Hayo yameelezwa tarehe 29 Septemba, 2025 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, wakati wa ziara yake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida.
Wakili Mpanju amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wazee katika taifa na itaendelea kuhakikisha wanapata huduma bora ikiwemo afya, makazi na ustawi wa kijamii.
“Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kuhakikisha wazee wanapata huduma bora na stahiki, ili waendelee kushiriki katika shughuli za kijamii na kuchangia uchumi wa taifa.” amesema Wakili Mpanju.
Aidha, Wakili Mpanju alikabidhi zawadi kwa wazee hao ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho hayo, ambapo zawadi hizo zilitolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni pamoja na mbuzi, maji, mchele, mafuta ya kupikia pamoja na televisheni, vitakavyosaidia wazee hao kusherehekea pamoja na kufuatilia matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Mbali na hayo, Wakili Mpanju ametoa wito kwa familia na jamii kuhakikisha wazee hawatengwi wala kusahaulika, bali washirikishwe kikamilifu katika shughuli za kijamii na kisiasa.
“Ni muhimu wazee wetu washiriki katika uchaguzi mkuu ujao kwa kupiga kura kwa kuwa ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kushiriki uchaguzi na kuchagua viongozi wanaowataka. Hivyo ni jukumu letu kuhakikisha wazee wanatimiza haki hii muhimu.” ameongeza Wakili Mpanju.
Nao baadhi ya Wazee wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwakumbuka na kuwathamini,huku wakibainisha kuwa hatua hiyo imewapa faraja na kuwahamasisha kushiriki katika maendeleo ya Taifa.
Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani hufanyika Oktoba 1 kila mwaka, yakilenga kutambua mchango wa kundi hilo na kuhamasisha jamii kuendelea kuliheshimu, kulilinda na kulipatia huduma bora.