Featured Kitaifa

DK.SAMIA AAHIDI FURSA ZAIDI KWA WAVUVI,WAFUGAJI PANGANI

Written by Alex Sonna

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Pangani katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM mkoani Tanga tarehe 29 Septemba, 2025.

….

MGOMBEA  wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kuwawezesha wavuvi na wafugaji wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga kupitia upatikanaji wa mikopo na masoko ya uhakika kwa bidhaa zinazozalishwa na sekta hizo.

Akihutubia wananchi wa Pangani leo Septemba 29, 2025)wakati wa kampeni zake mkoani humo, Dk. Samia amesema kuwa tayari serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa soko la samaki la kimataifa katika Kata ya Kipumbwi.

“Gharama za mradi huo ni Sh bilioni 1.3, ambazo zinajumuisha pia ujenzi wa vifaa vya kukaushia dagaa. Lengo ni kuongeza fursa za kiuchumi na kipato kwa wavuvi wetu,” amesema Dk.Samia

Aidha, Dk. Samia amesisitiza wafugaji kuchangamkia ruzuku za chanjo zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita, ikiwemo chanjo za kuku zinazotolewa bure, na ruzuku ya nusu bei ya chanjo za mbuzi na ng’ombe kwa nchi nzima.

Amebainisha kuwa chanjo hizo zinasaidia kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na wanyama hai katika soko la kimataifa, hivyo kuongeza kipato cha wafugaji na kukuza uchumi wa taifa.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Pangani katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi kwa CCM mkoani Tanga tarehe 29 Septemba, 2025.

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso mara baada ya kuwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Pangani mkoani Tanga tarehe 29 Septemba, 2025.

Matukio mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Pangani mkoani Tanga tarehe 29 Septemba, 2025.

Shamra shamra za wananchi wa Pangani mkoani Tanga katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) tarehe 29 Septemba, 2025.

About the author

Alex Sonna