Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo Septemba 28, 2025 ametoa ahadi ya Upanuzi kwenye maegesho ya Kivuko cha Magogoni na Kigamboni, lengoa ikiwa ni kuondoa foleni pamoja na kuboresha huduma katika kivuko hicho.
Dkt Nchimbi ametoa ahadi hiyo leo akizungumza na Wananchi wa Kigamboni katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Urais kuelekea Oktoba 29.
“Lakini vile vile katika miaka hii mitano, tumedhamiria kuhakikisha matengenezo ya Vivuko vyetu vya MV Magogoni na MV Kigamboni yanafanyika haraka” amesema Dkt Nchimbi.
Dkt Emmanuel John Nchimbi ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi mkuu wa 2025 wakipeperusha Bendera ya CCM, ambapo mkoa wa Dar es Salaam unakuwa wa 15 kufikiwa na Dkt Nchimbi katika kusaka kura za Ushindi kwa Chama hicho Tawala.