CHAKACHAKE, PEMBA – Shamra shamra na shangwe za maelfu ya wananchi na wapigakura wa Wilaya ya Chake Chake na vitongoji jirani zilitawala leo Jumamosi, Septemba 20, 2025, wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipowasili katika Viwanja vya Gombani ya Kale, Mkoa wa Kusini Pemba.
Aidha, katika mkutano huo wa hadhara, Dkt. Samia anatarajiwa pia kuwaomba kura wananchi na kuwanadi wagombea wa CCM wa nafasi za Uwakilishi na Ubunge kutoka Visiwani humo, ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Pemba na Tanzania kwa ujumla.
Viwanja vya Gombani ya Kale vilifurika watu wa rika zote, huku wakiashiria mshikamano na hamasa kubwa ya kisiasa kuelekea uchaguzi huo, ambapo wananchi wengi walionekana wakiwa na mabango, bendera na mavazi ya kijani na njano, rangi zinazotambulisha Chama Cha Mapinduzi.