Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu, ameandika historia kwa kuipa nchi medali ya kwanza ya dhahabu katika mashindano ya dunia ya riadha yanayoendelea jijini Tokyo, Japani.
Simbu aling’ara kwenye mbio hizo kwa kukimbia muda wa saa 2:09:48, na kufanikiwa kumshinda mpinzani wake mkali kutoka Ujerumani, Amanol Petros, kwa tofauti ndogo ya sekunde 0.03 pekee.
Ushindi huu wa kihistoria unaweka jina la Tanzania kwenye ramani ya dunia ya riadha na kumfanya Simbu kuwa shujaa mpya wa michezo nchini.