MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amepokewa kwa shangwe na Wananchi Kata ya Ndungu, Jimbo la Same Mashariki,alipowasili katika uwanja wa kata hiyo kwenye mkutano wake wa mwisho wa kampeni Mkoani Kilimanjaro leo Jumapili Septemba 14,2025.
Dkt.Nchimbi aliwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Mashariki,Ndugu Anne Kilango Malecella pamoja na Madiwani.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu na Makamu Wa Rais mstaafu Mzee John Samuel Malecela ambaye ni mume wa Mama Anne Kilango.