Na Gideon Gregory, Dodoma
Mgombea Urais wa Chama cha United Democratic Party (UDP), Mhe. Saum Hussein Rashid akiwa na mgombea mwenza Mhe. Juma Khamis Faki, leo Agosti 15, wamechukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais na makamu wa rais katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma, na kuwa chama cha 16 kufanya hivyo.
Baada ya kukabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, Mhe. Saum ameeleza kuwa endapo UDP itashinda itaenda kuwajaza mapesa watanzania ili waweze kujikomboa kiuchumi.
“Tutawajaza fedha watanzania kwa kufungua fursa mbalimbali katika sekta za kilimo, kuboresha miundombinu pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu katika sekta ya elimu.
Tunaposema kuwajaza mafedha watanzania tuna maana ni kuweka miundombinu mizuri kwa wananchi waweze kupata fedha ambazo zitawainua kiuchumi, kwa mfano zao la Pamba walime kisasa,”amesema
Aidha, amesema watafanya kilimo chenye tija kwa kufungua fursa zitakazopelekea biashara kufanyika kwa urahisi.