Featured Kitaifa

DKT.SAMIA NA DKT.NCHIMBI WAFUNGUA RASMI MBIO ZA URAIS,WACHUKUA FOMU INEC

Written by Alex Sonna

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Begi lenye Fomu zake za kugombea nafasi hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 09 Agosti, 2025.

Na Alex Sonna, Dodoma

MGOMBEA  wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea mwenza , Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo Agosti 9, 2025, wamefungua rasmi pazia la mchakato wa uchaguzi kwa kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) jijini Dodoma.

Dkt. Samia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, aliwasili katika ofisi hizo saa 11:15 asubuhi akiwa ameambatana na viongozi waandamizi wa chama hicho, akiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mizengo Pinda. Zoezi la uchukuaji wa fomu lilidumu kwa takribani dakika 28 hadi kukamilika.

Mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kuchukua fomu, Dkt. Samia na Dkt. Nchimbi walitoka nje ya jengo hilo na kuwaonesha waandishi wa habari mkoba maalum uliokuwa na fomu hizo, huku wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama waliowasindikiza.

Wakiwa na nyuso za furaha na bashasha, viongozi hao waliondoka katika eneo hilo saa 11:43 asubuhi, huku Dkt. Samia akiwapungia mkono viongozi na wafuasi wa CCM waliokuwepo kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Begi lenye Fomu za kugombea nafasi ya Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 09 Agosti, 2025. Kushoto ni Mgombea Mwenza Dkt. Emmanuel John Nchimbi

 

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Begi lenye Fomu zake za kugombea nafasi hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma tarehe 09 Agosti, 2025. 

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Wilaya ya Chamwino waliojitokeza kumuunga mkono tarehe 09 Agosti, 2025 wakati akielekea katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa ajili ya kuchukua Fomu ya kugombea nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 29 Oktoba, 2025. Pia wananchi hao walimchangia kiasi cha Shilingi Laki Mbili na Nusu ili zimsaidie kulipia fomu hiyo.

About the author

Alex Sonna