KATIBA wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makala,akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 25, jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum.
Na.Alex Sonna-DODOMA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu Maalum kwa njia ya mtandao kesho, Julai 26, 2025, ambapo ajenda kuu itakuwa kufanya marekebisho madogo ya Katiba ya chama hicho
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makala, amesema hayo leo Julai 25, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano huo mkuu maalum.
CPA Makala, amesema kumekuwepo na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao.
“Maneno mengi yamekuwepo kwenye mitandao watu wanauliza mkutano mkuu unakwenda kufanya nini sasa niwaambie tuu ajenda ya mkutano huu maalum ni moja tuu ambayo ni mabadiliko madogo ya katiba ambayo hayawezi kufanywa na kilao chochote zaidi ya mkutano mkuu.
“Mabadiliko ya katiba hayawezi kufanywa na Halmashauri Kuu wala Kamati Kuu wala vikao vya Sekretarieti bali ni wenye katika yao ambao ni mkutano mkuu”amesema Makala
Pia, amesema kwamujibu wa katiba ya Chama cha Mapinduzi CCM, inawaruhusu kufanya mkutano mkuu maalum kwa njia ya mtandao pale wanapoona inafaa.
Vile vile, amesema hadi sasa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwa mara ya kwanza watu watakwenda kushuhudi chama hicho kikifanya mkutano mkuu wake kwa njia ya mtandao.
“Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100, wilaya zipo tayari mikoa yote ipo tayari Sekretarieti tunaendelea na maandalizi ili kufanikisha mkutano huu mkuu maalum ambao utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM,”amesema Makala