Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, akipewa maelezo na Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Amri Matole, kuhusu takwimu rasmi na mchango wake katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Joseph Kuzilwa (kushoto), akipokelewa na Afisa Habari Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhan Kissimba, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya.

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Joseph Kuzilwa (katikati) na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo Vijijini na Mipango Miji wa Chuo hicho,Bw. Africanus Sarwatt, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Prof. Geradine Rasheli, akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Hazina Saccos, Dkt. Festo Mwaipaja, akipewa maelezo kuhusu Mifumo ya Fedha kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Tehama, Bi. Zaina Mwanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa akiteta jambo na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa TIB Development Bank, Joseph Chilambo (wa pili kushoto), wakisikiliza maelezo kuhusu Benki hiyo katika kuchochea maendeleo ya uchumi, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam
(Picha na Kitengo cha MawasilSerikalini, Wizara ya Fedha)
………..Na. Peter Haule,WF, Dar es Salaam
Tume ya Mipango itaendelea kushirikiana na Wizara ya Fedha na Taasisi zake katika utekelezaji na ufuatiliaji wa Dira ya Maendeleo 2050 kwa kuwa kazi nyingi za Tume hiyo zinategemea matokeo ya kazi zinazofanywa na Wizara hususani Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa,
alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa Takwimu mbalimbali za kiuchumi, kijamii na mazingira zitasaidia katika kupanga, kupima, kufuatilia na kufanya tathmini ya programu za maendeleo wakati wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.
Dkt. Msemwa alisema kuwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050,Tume itahitaji takwimu na viashiria muhimu vya mara kwa mara kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikiwa ni pamoja na takwimu rasmi katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya idadi ya watu, pato la taifa na viasihiria vingine vya kiuchumi na kijamii ukiwemo mfumuko wa bei.
Aidha, viongozi mbalimbali wa Taasisi na Idara wameendelea kutembelea Banda la Wizara ya Fedha akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Joseph Kuzilwa.
Viongozi wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Prof. Geradine Rasheli, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza na Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Ruth Minja.
Wengine ni Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo, Kaimu Mkurugenzi wa TIB Development Bank, Joseph Chilambo, Mkurugenzi wa Hazina Saccos, Dkt. Festo Mwaipaja, Msajili Baraza la Masoko ya Mitaji, Bw. Martin Kolikoli na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Dkt. Kedmon Mapama.
Wizara ya Fedha kupitia Idara na Vitengo lakini pia Taasisi zilizo chini ya Wizara, inaendelea kuwakaribisha watanzania kutembelea Banda la Wizara hiyo ili waweze kuhudumiwa.