Featured Kitaifa

TAARIFA ZA UCHUMI TANGU UHURU ZAPATIKANA KWENYE MFUMO WA HAZINA MACHAPISHO

Written by mzalendoeditor
Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Prof. Sylivia Temu akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkutubi Mwandamizi  wa Kitengo cha Maktaba Wizara ya Fedha, Bw. Fredy Mpoma, kuhusu Mfumo wa Hazina Machapisho wenye taarifa za uchumi tangu kupata uhuru alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Sylivia Temu, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi kuhusu miradi mikubwa inayoweza kutekelezwa kwa ubia, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi wa Idara Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo,  akisikiliza maelezo kutoka kwa Bw. Stanslaus Mpembe, kuhusu masuala mbalimbali ya huduma za fedha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na TEHAMA, Bw. Charles Maganga, akitoa elimu kwa Bw. Ali Sultan, kuhusu mifumo ya fedha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam
Mchumi Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Samweli Mkwama, akitoa elimu kwa Bw. Alex Mwambenja kuhusu matumizi ya Bajeti iliyopitishwa na Bunge katika miradi ya maendeleo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mkutubi Mwandamizi  wa Kitengo cha Maktaba Wizara ya Fedha, Bw. Fredy Mpoma, akitoa elimu kuhusu Mfumo wa Hazina Machapisho wenye taarifa za uchumi tangu kupata uhuru kwa Bw. Gabriel Wenslaus, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Wataalamu kutoka Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha, wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha).
……….
Na. Peter Haule na Joseph Mahumi ,WF, Dar es Salaam
Mfumo wa Hazina ya Machapisho (Mof respository) ni muhimu kwa wananchi katika kujua taarifa za uchumi na fedha kuanzia nchi ipate uhuru hadi sasa.
Hayo yamesemwa na Mkutubi Mwandamizi wa Kitengo cha Maktaba Wizara ya Fedha, Bw. Fredy Mpoma, alipokuwa akitoa elimu katika Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Bw. Mpoma alisema kuwa Mfumo huo ambao ni muhimu katika uhifadhi na upatikanaji wa taarifa za Wizara ya Fedha tangu uhuru unasaidia katika kuongeza ufahamu wa wapi uchumi umetoka na unakoelekea kupitia mtiririko wa taarifa mbalimbali.
Alibainisha machapisho yanayopatikana katika Mfumo huo kuwa ni Bajeti, Hali ya Uchumi, Deni la Taifa na Sheria ya fedha tangu uhuru.
Alisema machapisho hayo yanasaidia kuboresha utendaji na ufahamu wa masuala ya uchumi na kuwa na mipango yenye kuzingatia uhalisia kwa kutambua hatua kubwa iliyofikiwa na Serikali katika kuimarisha uchumi hadi sasa.
Alisema kuwa kizazi cha sasa hakina taarifa ya kutosha kuhusu mwenendo wa uchumi tangu uhuru, hivyo kupitia Mfumo huo ni wazi kwamba vijana wanaweza kuwa na hoja za msingi wanapo fuatilia maendeleo ya kiuchumi na hatua ambayo Tanzania imepiga ikilinganishwa na nchi nyingine hususani za Afrika.
Bw. Mpoma alisema kuwa hapo awali ilikuwa vigumu kwa taasisi za elimu ambazo zinajukumu la kufanya tafiti za kitaaluma kupata taarifa kwa usahihi na kwa wakati kuhusu hali ya uchumi na bajeti lakini kwa sasa kwa kutumia mfumo huo imerahisisha kupata taarifa katika kuboresha majukumu yao.
Aidha, ametoa rai kwa wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Fedha katika maonesho hayo ili kupata taarifa za kina kuhusu mfumo huo ambao unaweza kupatikana kwa kutumia vifaa mbalimbali vya kielektroniki zikiwemo simu janja za mkononi.

About the author

mzalendoeditor