Featured Michezo

‘VIBE’ MAHUSIANO SPORTS BONANZA RAHA TUPU MSALALA

Written by mzalendoeditor
Wachezaji wa timu ya Lwabakanga na Kakola wakiwania mpira katika moja ya mchezo.
Kikosi cha timu ya Bugarama katika picha ya pamoja kabla ya mchezo
Wachezaji wa timu za Bugarama na Busindi wakisalimiana kabla ya mechi yao kuanza.
Wachezaji wakiwa uwanjani kabla ya mechi kuanza
Ukitembelea kata mbalimbali zinazozunguka Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu uliopo halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kipindi hiki, utakuta viwanja vya michezo vimejaa watu wakishuhudia michuano ya soka ya mashindano ya Mahusiano Sports Bonanza yaliyozinduliwa hivi karibuni.
Mashindano haya ya Mahusiano Sports yanayofadhiliwa na Barrick Bulyanhulu yanashirikisha timu 16 za vijana kutoka vijiji 16 kutoka kata 3 za Bugarama,Bulyanhulu na Mwingiro kwa hivi sasa ziko katika hatua ya kutoana kabla ya kuingia katika hatua ya robo fainali.
Baadhi ya mechi zilizochezwa zilizokuwa na ushindani mkubwa ni Kati ya Kakola na Lwabakanga ambapo timu ya Lwabakanga ilifanikiwa kushinda mchezo huo kwa Penati 3- 2 baada ya timu hizo kutofungana ndani ya dakika 90, Lwabakanga imefuzu kuingia katika hatua ya nane bora.
Katika Mchezo mwingine uliochezwa katika kata ya Bugarama ilizikutanisha timu za Bugarama na Busindi, ambapo Busindi ilishinda kwa bao 1 kwa 0 dhidi ya Bugarama na kufanikiwa kufuzu kuingia hatua inayofuata ya nane bora ikiungana na timu ya Lwabakanga.
Akiongea wakati wa uzinguzi wa mashindano hayo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Johan Labuschagne alisema mgodi utaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza michezo na kuibua vipaji, pia aliongeza kuwa michezo na ,mabonanza ya pamoja ni moja ya jukwaa la kukuza uhusiano mwema baina ya Mgodi na jamii inayouzunguka.
Baadhi ya wakazi wa kata hizo wameupongeza mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuanzisha ma kufadhili ligi hiyo ya vijana kwa kuwa mbali na kuleta burudani kwa wananchi mashindano hayo yanasaidia kuwajenga vijana kiafya sambamba na kuwaepusha kujihusisha na vitendo viovu katika jamii.
Mashindano hayo yapo kwenye hatua ya makundi ambapo timu 16 zitachuana mpaka kupata timu 8 zitakazoingia hatua ya robo fainali kisha timu 4 kucheza nusu fainali na kisha kupatikana timu 2 zitazocheza fainali.

About the author

mzalendoeditor