MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt.James Andilile,akizungumza na waandishi wa habari katika banda la EWURA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna _DODOMA
KATIKA kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2025, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesisitiza dhamira yake ya kutoa huduma bora, zenye kuzingatia weledi, uwazi, uwajibikaji na matumizi bora ya teknolojia kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Akizungumza katika maadhimisho hayo jijini Dodoma June 16,2025 Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile amesema EWURA itaendelea kujielekeza katika kuwahudumia wananchi kwa ufanisi na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, kwa kuhakikisha kuwa huduma zote za nishati na maji zinafikia walengwa kwa ubora unaostahili.
“Huduma kwa wananchi siyo fadhila, ni haki yao ya msingi,kama Taasisi ya Serikali, tunatambua wajibu wetu kwa Watanzania na ndiyo maana tunaendelea kujipanga kutoa huduma bora kwa kutumia mifumo ya kidijitali na kuimarisha usimamizi katika sekta tunazozihudumia,” amesema .
Ameongeza kuwa katika kipindi cha wiki ya utumishi wa umma, EWURA imekuwa ikikutana moja kwa moja na wananchi ili kusikiliza changamoto, kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wao, na kueleza namna taasisi hiyo inavyosimamia bei, ubora, na upatikanaji wa huduma za mafuta, umeme, gesi asilia, na maji safi na usafi wa mazingira.
Aidha, amesema EWURA inatambua kwamba huduma bora kwa umma ni chachu ya ustawi wa jamii na uchumi wa nchi, hivyo itaendelea kusimamia misingi ya utawala bora ikiwemo uwazi, uwajibikaji na kushirikisha wananchi katika maamuzi.
Katika hatua nyingine, Dkt.Andilile ametoa wito kwa jamii kuhakikisha wanatumia wiki ya utumishi kama jukwaa la kupata taarifa mbalimbali za EWURA na kueleza kuwa hali hiyo itaboresha mifumo ya utoaji huduma na kujifunza kutoka kwa wadau na wananchi.
Aidha amesisitiza kuwa EWURA iko tayari kuwachukulia hatua kali wafanyabiashara wa vituo vya mafuta ya Taa, petroli au dizeli watakao fanya bishara kea kuchakachuo bidhaa hizo.
Pia wafanya bishara hao wametakiwa kuzingatia bei elekezi kwa kumuuzia mafuta mteja kadri ya mahitaji yake na si vinginevyo.
Wiki ya Utumishi wa Umma huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha uwajibikaji, maadili ya kazi, pamoja na kutoa nafasi kwa taasisi za umma kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika upatikanaji wa huduma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile,baada ya kutembelea banda EWURA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt.James Andilile,mara baada ya kutembelea banda la EWURA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt.James Andilile,akizungumza na waandishi wa habari katika banda la EWURA wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.