Featured Michezo

MGODI WA BARRICK BULYANHULU WADHAMINI MAHUSIANO SPORTS BONANZA MSALALA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akicheza mpira wakati wa ufunguzi wa Mahusiano Sports Bonanza

Meneja Mkuu wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Johan Labuschagne akicheza mpira wakati wa ufunguzi wa Mahusiano Sports Bonanza

Meneja Mkuu wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Johan Labuschagne akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mahusiano Sports Bonanza
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mahusiano Sports Bonanza
Katika dhamira yake ya kukuza michezo na kujenga uhusiano mzuri na jamii,mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya Msalala umefadhili bonanza la michezo lijulikanalo kama Mahusiano Sports Bonanza.
Bonanza hilo ambalo limezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mboni Mhita,limeanza kwa shamra shamra za michezo mbalimbali iliyohusisha wananchi kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi na Wafanyakazi wa Mgodi.
Bonanza hilo linashirikisha timu 16 kutoka katika vijiji 16 vilivyopo katika kata 3 zinazozunguka Mgodi huo.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo,DC Mboni Mhita ameupongeza Mgodi wa Bulyanhulu kwa uamuzi wa kujikita kudhamini michezo mbali na kazi nzuri unaofanya kwa kushirikiana na Serikali ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii.
Amesema mbali na michezo kuwa burudani inadumisha uhusiano mzuri katika jamii sambamba na kujenga afya.
Hafla ya ufunguzi wa bonanza hilo imefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kakola halmashauri ya Msalala na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani kutoka katika kata hizo tatu zinapotoka timu shiriki ambao wamesema wanajivunia uwepo wa Mgodi huo kwenye wilaya yao.
Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Johan Labuschagne amesema Bonanza hilo linashirikisha timu 16 kutoka katika kata 3 za Bugarama, Bulyanhulu na Mwingiro ambapo Mshindi wa Bonanza hilo atazawadiwa Kikombe pamoja na zawadi nyingine na kila timu itapatiwa jezi na mpira.
Amesisitiza kuwa Mgodi utaendelea kuandaa mabonanza kama hilo kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha sekta ya michezo mbalimbali nchini.
Awali kabla ya uzinduzi wa bonanza hilo kulifanyika michezo mbalimbali kama kuvuta Kamba, kukimbiza kuku , kucheza muziki kwa ajili ya kuwaburudisha wananchi huku zawadi Mbalimbali zikitolewa kwa Washindi na wananchi
Huu ni utaratibu wa kawaida kwa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wa kuandaa na kushiriki katika Mabonanza mbalimbali kwa lengo la kuwakutanisha Wananchi na Wafanyakazi wa Mgodi huo.
Kauli Mbiu ya Bonanza la mwaka huu inasema “UMOJA NA FURAHA KWA JAMII YA BULYANHULU , PIGA MPIRA JENGA MAHUSIANO”

About the author

mzalendoeditor