Featured Kitaifa

BALOZI NCHIMBI ZIARANI MKOA WA SIMIYU

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Masanja Michael Lushinge (smart) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndugu Said Mtanda, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Dkt Nchimbi, alikuwa safarini kuelekea Mkoa wa Simiyu kwa ziara ya kikazi ambako anatarajiwa kushiriki kongamano la Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT). 

Akiwa uwanjani hapo, Balozi Nchimbi pia alikutana na kusalimiana na Mama Janeth Magufuli, mjane wa hayati Rais John Pombe Magufuli.

About the author

mzalendoeditor