Featured Kitaifa

WANACHAMA WA VYAMA VYA USHIRIKA VYA MAZAO YA BUSTANI MIRERANI WAPATIWA MAFUNZO

Written by mzalendoeditor

MRAJIS Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara, Absalom Cheliga,akizungumza wakati akifungua  Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

AFISA Ushirika Mwandamizi kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Bi.Happyness Olotu,akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

AFISA Ushirika Mkuu  Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) ,Justin Mogendi,akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

AFISA  Ushirika Wilaya ya Simanjiro, Moses Kaaya ,akizungumza wakati wa Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

SEHEMU ya washiriki wakisikiliza mada mbalimbali wakati wa  Mafunzo kwa Wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani ikiwa ni utekelezaji wa Mradi kwa awamu ya pili Mwaka 2024/25 yaliyofanyika leo Juni 2,2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

…….
WANACHAMA wa Vyama vya Ushirika wa mazao ya Bustani Mkoani Manyara  wanaojishughulisha na kilimo cha matunda na mbogamboga  wamepatiwa mafunzo katika nyanja mbalimbali za  uzalishaji wenye tija, masoko  na uwekezaji kwenye shughuli zao.
Mafunzo hayo hayo yametolewa leo Juni 2, 2025 Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara na  Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara, Absalom Cheliga, ikiwa ni utekelezaji wa Mradi huo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Cheliga amesema  moja ya kati ya kazi  muhimu kwao ni pamoja na kuwajengea uwezo wanachama  ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na kujiongezea kipato.
Amesema lengo ni Wanaushirika kuongeza tija katika uzalishaji pamoja na kuiishi dhana ya ushirika, uzalishaji wa tija wakiwa shambani, masoko na uwekezaji kwenye shughuli zao.
“Natoa wito kwa jamii kujiunga na vyama vya ushirika kwa sababu ni nyenzo muhimu katika ushirikiano Pamoja na kuweza kujiongezea kipato,”amesema Cheliga
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa AMCOS  Mirerani, George Lyimo amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwaletea mafunzo hayo ambayo yamezidi kuwaongezea maarifa kwani Amcos yao ya Mirerani ni mpya.
“Kupitia mafunzo haya wanachama wataenda kupiga hatua na ni  matumaini yetu serikali yetu ipo pamoja na sisi na sisi viongozi tuliopata mafunzo  awamu ya kwanza na haya yamekuwa ni ya awamu ya pili, tunaishukuru Serikali kwa kuweza kutufikia,” amesema Lyimo.
Afisa Ushirika Wilaya ya Simanjiro, Moses Kaaya amesema  chama hicho kilianzishwa  Februari  mwaka jana ambapo  kwa kipindi hicho wanachama wamepata mwitikio mkubwa kwani awali walikuwa  20 lakini  kwa sasa wapo  100.
Amesema  kupitia uongozi Madhubuti  wameweza kuanzisha biashara ya mbolea  kwa kuleta huduma karibu na wakulima.
Amesema  changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili ni mafuriko lakini Seriakli imeweza kutatua kwa kuchimba mfereji mkubwa na wakulima wanaendelea na shughuli za kilimo Januari hadi Disemba.

About the author

mzalendoeditor