Featured Kitaifa

MAJALIWA: MAPINDUZI MAKUBWA YAMEFANYIKA KATIKA SEKTA YA MICHEZO

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha tuzo ya pongezi na shukurani za dhati ya kutambua mchango wake katika kuendeleza michezo nchini alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam, Juni 1, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

….

*Asema utoaji wa tuzo unalenga kuendeleza na kuimarisha sekta ya michezo nchini

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya michezo kama sehemu ya utekelezaji wa Ibara ya 243 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.

Pia, Waziri Mkuu ametaja mafanikio yaliyopatika katika sekta ya michezo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka shilingi bilioni 285 mwaka 2024/2025 hadi bilioni 519 katika mwaka wa fedha 2025/2026. “Ongezeko hili ni kubwa zaidi katika historia ya Wizara hii.”

“…Serikali imeendelea na mkakati wake wa kuhakikisha inainua michezo hapa nchini, kila mmoja kwa nafasi yake uwe mchezaji, wakala, mdhamini endelezeni taaluma hiyo. Leo hii tuna kila sababu ya kumpongeza na kumshukuru rais wetu kwa kufungua hiyo milango na kuongeza bajeti na kuruhusu sekta binafsi kushiriki kwenye michezo.”

Ameyasema hayo jana usiku (Jumapili, Juni Mosi, 2025) katika hafla ya usiku wa tuzo zilizoandaliwa na Baraza la Michezo Tanzania kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa iliyofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam.

Amesema uwepo wa tuzo kwa wanamichezo ni hatua muhimu yenye malengo mahususi na manufaa makubwa katika kuendeleza na kuimarisha sekta ya michezo nchini ikiwa ni pamoja na kuwapa wachezaji motisha ya kuongeza juhudi katika mafunzo, nidhamu, na utekelezaji wa majukumu na hivyo kuboresha viwango vya michezo kitaifa na kimataifa.

“Tuzo hizi hazifanyiki kwa ajili ya sherehe tu, bali ni sehemu ya mkakati wa kuhamasisha maendeleo ya michezo. Nitumie fursa hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya malengo na manufaa ya kuwa na tuzo hizi”

Waziri Mkuu, alisema tuzo hizo pia zinalenga kuwatia moyo na kutambua kazi kubwa inayofanywa na wanamichezo, makocha, timu na wadau wengine katika kuiwakilisha na kuiinua nchi yetu kimataifa, kuchochea na kuibua ari ya ushindani chanya miongoni mwa wanamichezo na kutoa motisha kwa watoto kuingia kwenye michezo.

“Kwa kuwa michezo ni afya, ajira, burudani na mshikamano; tuzo hupeleka ujumbe kwa jamii kwamba michezo ni shughuli ya heshima na ya maendeleo. Hii husaidia hata wazazi na jamii kwa ujumla kuwahamasisha watoto kushiriki michezo.”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa alisema tuzo hizo ni chachu ya maendeleo ya michezo ambazo zinatoa matumaini, zinajenga heshima, na kuimarisha mustakabali wa michezo nchini. Tunapaswa kuzidumisha, kuziboresha na kuzitumia kama sehemu ya mchakato wa kuendeleza sekta hii muhimu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi alitumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuendeleza sekta ya michezo nchini. “Sote ni mashuhuda wa jitihada kubwa za Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha kuwa sekta ya michezo inapiga hatua.”

Alisema sekta ya michezo imeshuhudia mafanikio makubwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita. “Kwa mara ya kwanza tunazishuhudia timu za Tanzania za michezo mbalimbali zikicheza kombe la dunia, hali kadhalika timu za vilabu hususan vya Mpira wa Miguu zimeweza kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika.” 

Awali, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Neema alisema lengo la utoaji wa tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa msimu wa tatu ni kuwatambua wanamichezo wote waliofanya vizuri katika Nyanja za kimataifa.

Katibu huyo wa BMT alisema kwamba mchakato wa kuwapata washindi wa tuzo hizo ulipitia katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushirikisha vyama na mashirikisho ya michezo ambayo yanatambulika.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi  kwa naiba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Haasan tuzo ya pongezi na shukurani za dhati kwa mchango wa Rais katika kuendeleza michezo nchini, alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam, Juni 1, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi   tuzo ya pongezi na shukurani za dhati kwa mchango wake katika kuendeleza michezo nchini, alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam, Juni 1, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha tuzo ya pongezi na shukurani za dhati ya kutambua mchango wake katika kuendeleza michezo nchini alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam, Juni 1, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki  jijini Dar es Salaam, Juni 1, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa hafla ya  utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa kwenye ukumbi wa Super Dome jijini Dar es salaam, Juni 2, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Waziri wa Habari, Utamaduni Sana na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, Leodgar Tenga (kulia)  wakifurahia burudani  katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki  jijini Dar es Salaam, Juni 2, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi alipowasili kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki  jijini Dar es Salaam kumwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es salaam, Juni 1, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mchezaji wa Kimataifa wa soka la wanawake, Aisha Masaka aliyeibuka  mshindi wa jumla upande wa wanawake  katika Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es salaam, Juni 1, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Bondia, Fadhili Majiha aliyeibuka  mshindi wa jumla upande wa wanaume katika tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo iliyoandaliwa na BMT kwenye ukumbi wa The The Super Dome Masaki jijini Dar es salaam, Juni 1, 2025.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendoeditor