Featured Kitaifa

WIZARA YA MAJI YATAJA VIPAUMBELE SABA

Written by mzalendoeditor
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwasilisha leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026 .
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwasilisha leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026 .
…..
WIZARA ya Maji imetaja vipaumbele  vyake saba katika mwaka wa fedha 2025-2026 ikiwemo kuzuia upotevu wa maji.
Vipaumbele hivyo vimetajwa leo bungeni na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Aweso ametaja vipaumbele vingine ni kusimamia Usimamizi wa rasilimali za Maji,kuendeleza rasilimali maji,Usimamizi wa huduma ya ubora wa Majisafi na Majitaka.
Pia,huduma za usambazaji wa Maji katika maeneo ya mijini,huduma za Maji safi na Majitaka katika maeneo ya mijini.
Vipaumbele vingine ni kudhibiti upotevu wa maji na kujenga uwezo wa kitaasisi ili Wizara iweze kujiendesha.

About the author

mzalendoeditor