Featured Kitaifa

WANANCHI KUREJESHEWA HUDUMA YA MAJI,SERIKALI YATANGAZA MSAMAHA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akiwasilisha leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025-2026 .

…..

WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ametangaza msamaha wa faini zote kwa wananchi waliokuwa wakidaiwa na Mamlaka za Maji nchini, hatua inayolenga kuwapunguzia mzigo wa gharama na kuwawezesha kurejeshewa huduma za maji.

Msamaha huo umetangazwa na leo Mei 8,2025 bungeni jijini Dodoma na Mhe.wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

“Ninapenda kutoa salamu za wizara kwa wananchi wote wenye faini kuwa Mama Samia Suluhu Hassan amesamehe faini hizo. Wafike katika Mamlaka za Maji kuanzia sasa hadi Mei 31, 2025, ili kupewa utaratibu wa kurejeshewa huduma ya maji,” amesema Aweso.

Pia amesisitiza kuwa wateja wote waliokatiwa maji kutokana na madeni, wanatakiwa kufika katika ofisi za mamlaka husika ili kupewa utaratibu wa ulipaji wa madeni yao na kurejeshewa huduma.

 “Maunganisho ya maji kwa wateja wapya yafanyike ndani ya siku saba, kwa mujibu wa miongozo ya Wizara.”

Aidha Waziri Aweso ameagiza kuwa huduma ya maji isikatwe katika kipindi cha sikukuu au mwishoni mwa wiki. 

About the author

mzalendoeditor