Featured Kitaifa

 TAWIFA YATOA MAFUNZO YA KIFEDHA NA BIASHARA KWA WANAWAKE ZAIDI YA 200 WANAOJIHUSISHA NA UJASIRIAMALI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji ,Bi.Aziza Mumba,akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa leo Aprili 12,2025  na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) kwa wanawake 200 wanaojihusisha na ujasiriamali  mkoa wa   Dodoma.

Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA),,Bi. Fikira Ntomola,,akizungumza wakati wa  mafunzo ya kifedha na kibiashara kwa wanawake 200 wanaojihusisha na ujasiriamali  mkoa wa   Dodoma leo Aprili 12,2025.

Sehemu ya washiriki wakifatilia mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa  na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA) kwa wanawake zaidi ya 200  Mkoa wa Dodoma wanaojihusisha na ujasiriamali.

Wakichangia 

…..

ZAIDI  ya wanawake 200 wanaojihusisha na ujasiriamali  mkoani  Dodoma wamepatiwa mafunzo ya kifedha na kibiashara yaliyoandaliwa na taasisi ya Chama wa Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA), ikiwa ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa wanawake wajasiriamali utakaofanyika Aprili 13,mwaka huu jijini Dodoma.
Akifungua mafunzo hayo leo April 12, 2025 jijini Dodoma Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji ,Bi.Aziza Mumba,amesema  kuwa mafanikio ya wajasiriamali wanawake yanategemea nidhamu ya fedha na matumizi sahihi ya maarifa ya kifedha.
“Biashara haiwezi kukua kama hakuna nidhamu ya fedha. Mafunzo haya ni muhimu kwa kila mjasiriamali anayetaka kuimarika kiuchumi katika Mkoa wa Dodoma ,” amesema Bi. Mumba
Aidha ameeleza kuwa benki nyingi ziko tayari kutoa mikopo, lakini zinahitaji kuona mwelekeo wa biashara na usimamizi mzuri wa mapato na matumizi ya mjasiriamali husika.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wanawake kwenye Sekta ya Fedha (TAWIFA),,Bi. Fikira Ntomola, amesema kuwa taasisi hiyo ilianzishwa mwaka jana kwa lengo la kuinua wanawake kiuchumi kupitia elimu ya fedha, uwekezaji, na usimamizi wa biashara.
“Tunahamasisha wanawake kuwekeza kwenye masoko ya mitaji na kuhakikisha wanakuwa na bima ya biashara zao kama kinga dhidi ya majanga,” amesema Bi. Ntomola.
Mafunzo hayo yamehusisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya fedha, wakiwemo wawakilishi wa benki waliotoa elimu kuhusu mikopo, marejesho, na fursa za kifedha zinazopatikana kwa wanawake wajasiriamali.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Mkoa wa Dodoma, Bi. Mary Barnabas, amesema kuwa wanawake waliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo ni sehemu ndogo ya zaidi ya wanawake 6,000 wanaojihusisha na ujasiriamali mkoani humo.
“Tunapaswa kuzingatia elimu tunayopewa. Tukiitumia vyema, biashara zetu zitakua na mitaji itaongezeka,” amesema 
Pia amesisitiza umuhimu wa wanawake kubadili tabia za kifedha, kuepuka matumizi yasiyopangwa kwenye bajeti, na kutumia rasilimali walizonazo kwa malengo ya maendeleo ya biashara.
Mafunzo hayo, yaliyoambatana na kauli mbiu “Huduma Jumuishi za Kifedha”, yamelenga kuwawezesha wanawake kupata mikopo kwa urahisi, kukuza mitaji yao, na kulinda biashara kupitia uwekezaji na bima.

About the author

mzalendoeditor