Featured Kitaifa

JAFO AKUNWA NA UWEKEZAJI KIWANDA CHA MAGODORO YA DODOMA ASILI,ATAKA WALIFIKIE SOKO LA AFRIKA

Written by mzalendoeditor
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akikagua na kujionea shughuli za uzalishaji katika  Kiwanda Cha  Magodoro ya Dodoma Asili  kilichopo katika eneo la Four Ways leo Aprili 10,2025 Jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) amewataka Wamiliki  wa Kiwanda Cha  Magodoro ya Dodoma Asili kuhakikisha wanalifikia Soko huru  la Afrika AfCFTA) katika uuzaji wa magodoro huku akifurahishwa na jinsi ambavyo wametoa  ajira kwa Watanzania pamoja na kukuza uchumi wa Nchi.
Kauli hiyo ameitoa leo Aprili 10,2025  wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho  kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji kilichopo katika eneo la Four Ways Jijini Dodoma.
Waziri Jafo amesema anafarijika  kuona uwekezaji mkubwa ambao umefanywa ambapo zaidi ya watumishi 130 wameajiriwa na  kiwanda hicho kinalipa Kodi ya zaidi ya Sh bilioni 3 kwa mwaka hivyo kuongeza tija katika uchumi wa Nchi
Amesema amefarika kwa jinsi ambavyo Shirika la Viwango (TBS)  linavyosimamia Viwango katika Kiwanda hicho.
“Nikiwa Waziri napata faraja kuona kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa  Rais Samia Suluhu Hassan inaenda vizuri.Niwaombe wawekezaji kuongeza spidi katika uzalishaji ili ikiwezekana kulifikia soko la Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
“Imani yetu tutaendelea kupambana kuhakikisha tunaendeleza uchumi wetu nimefarijiika hata kina dada wengi wamepata ajira hapa ,”amesema Waziri Jafo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma,Bi.Mwajabu Nyamkomola  amewapongeza wawekezaji wa Kiwanda hicho kwa kuweza kutoa ajira kwa watanzania ikiwemo na wanawake.
“Maendeleo yoyote ya Nchi yanategemea uchumi wa Viwanda,Serikali ya awamu ya Sita imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wetu.
Amesema wanaendelea kuhamasisha uwekezaji mkubwa Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuongeza uchumi wa wananchi wa eneo hilo.
Kwa upande wake mfanyakazi wa Kiwanda hicho, Tausi Mayonga amesema amefanya kazi kwa muda wa miaka 13 ambapo  amemshukuru  mwajiri wao kwa kutoa usawa katika suala la ajira.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akimsikiliza Meneja wa Kiwanda Cha  Magodoro ya Dodoma Asili Bw.Prashant Bhavsar wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho  kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji kilichopo katika eneo la Four Ways leo Aprili 10,2025 Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda Cha  Magodoro ya Dodoma Asili Bw.Prashant Bhavsar wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho  kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji kilichopo katika eneo la Four Ways leo Aprili 10,2025 Jijini Dodoma.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiendelea kutembelea na kujionea shughuli za uzalishaji katika  Kiwanda Cha  Magodoro ya Dodoma Asili  kilichopo katika eneo la Four Ways leo Aprili 10,2025 Jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor