Featured Kitaifa

DKT.BITEKO AIPONGEZA EWURA KUANDAA TAARIFA ZA MAENDELEO YA SEKTA YA NISHATI NCHINI

Written by mzalendoeditor
NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati akizindua  Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.
📌Asema taarifa hizo ni kioo cha kupima na kutathmini uwazi na ufanisi wa sekta hiyo 
📌Awataka wananchi kuzisoma taarifa hizo ili wapate majawabu ya hali ya utoaji wa huduma za umeme, mafuta na gesi asilia
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kwa kuandaa Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24 kwa kuwa zina umuhimu mkubwa kwa Serikali katika kufanya maamuzi.
Dkt.Biteko ametoa pongezi hizo leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma wakati akizindua uzinduzi wa Taarifa za hizo Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24.
“Leo ni kwa mara ya pili, tunazindua Taarifa tatu kwa pamoja ambazo ni za umeme, mafuta na gesi asilia, ambapo ni matokeo ya udhibiti na uchambuzi wa kina uliofanywa na EWURA. Taarifa hizi zinaonesha hali ya Sekta yetu ya Nishati, mafanikio, changamoto na fursa zilizopo katika kuendeleza sekta hii.”amesema Dkt.Biteko
Aidha amesema kuwa taarofa hizo pia zinasaidia wadau wengine wakiwemo wawekezaji, wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali katika Sekta ya Nishati kujitathmini, kuboresha utendaji, na wananchi kufahamu maendeleo yaliyofikiwa katika utoaji na upatikanaji wa huduma kwa undani zaidi.
Amesema kuwa Sekta ya Nishati ina umuhimu wa kipekee kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Bila nishati ya kutosha na ya uhakika ni vigumu kufikia malengo yetu ya maendeleo.
“Nishati ni kichocheo cha ukuaji wa viwanda, uboreshaji wa huduma za kijamii kama afya, maji na elimu na pia ni muhimu katika kuboresha maisha ya kila Mtanzania.”amesema Dkt.Biteko
Hata hivyo  ameipongeza Bodi ya EWURA pamoja na menejimenti kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya ya uthibiti katika sekta ndogo za mafuta, umeme na gesi asilia, na leo wametualika kwa ajili ya uzinduzi wa Sekta hizo.
Kwa upande wa sekta ndogo ya gesi asilia, Dkt. Biteko amesema kama zilivyo sekta nyingine za nishati kwa mujibu wa Taarifa hiyo, imeonesha kuwepo ongezeko la matumizi ya gesi asilia viwandani, majumbani na kwenye vyombo vya usafiri. Aidha, vituo vya kujaza gesi iliyoshindiliwa kwenye magari (CNG) vimeongezeka.
“Taarifa hiyo inaonesha kuimarika kwa upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na jitihada za kuhamasisha wawekezaji wa ndani kujenga vituo vya mafuta katika miji midogo na vijijini ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa hiyo. Aidha, amezipongeza kampuni za mafuta kwa kushirikiana vizuri na Serikali.”amesema  
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Mhe. Judith Kapinga,amesema  kuwa kwa kipindi cha miaka minne sasa Sekta hiyo imekuwa mashuhuri ndani ya nchi na nje kutokana na umadhubuti wa Rais Dk. Samia wa kuendeIea kuimarisha uwekezaji katika sekta hiyo.
“Naendelea kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa inayofanyika katika sekta ndogo ya nishati, na usimamizi mzuri wa Dkt. Biteko unaowezesha kupata mafanikio yote haya,” amesema Mhe. Kapinga.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA, Prof. Mark Mwandosya, ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa inaoendelea kuufanya katika sekta ya nishati.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile alisema kuwa uzinduzi wa taarifa hizo ni takwa la kisheria na tayari wameshafanya hivyo kwa upande wa sekta ya maji.
Amesema, katika sekta ndogo ya umeme hadi kufikia Juni 2023/2024 uzalishaji wa umeme ulikuwa megawati 2,411 na sasa umefikia megawati 4,032.
“Kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme huduma imeimarika na changamoto iliyokuwepo imeondoka kutokana na uwekezaji katika miundombinu, na hali ya kifedha ya TANESCO imeendelea kuimarika kwa mwaka wa tatu mfululizo ambapo imetengeneza faida kutokana na usimamizi wa Serikali wa kuondokana na mitambo ya kukodi ya kuzalisha umeme,” amesema Dkt.Andilile
Hata hivyo ameongeza  kuwa katika sekta ya mafuta hadi kufikia Juni 2024,  vituo vya mafuta vilikuwa 2,361 sawa na ongezeko la asilimia 10, kukiwa na vituo 480 vijijini sawa na ongezeko la asilimia 12. Pia, kuhusu gesi asilia amesema katika mwaka 2022/23,  vyombo vya moto vilivyokuwa vinatumia gesi asilia vilikuwa 7,000 na kufikia Machi mwaka huu, vimefikia 15,000 ikiwa ni sawa na asilimia 49.

NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati akizindua  Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati akizindua  Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akizungumza wakati akizindua  Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu   Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,(hayupo pichani)  wakati akizindua  Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Wizara ya Nishati, Mhe. Judith Kapinga,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA, Prof. Mark Mwandosya,akizungumza  wakati wa uzinduzi wa  Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile,,akizungumza  wakati wa uzinduzi wa  Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

NAIBU  Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akionesha Vitabu vya Taarifa mara baada ya kuzindua Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua (Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24,hafla iliyofanyika leo Aprili 9,2025 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor