Featured Kitaifa

HUDUMA ZA MACHO KUTOLEWA BURE WIKI YA AFYA.

Written by mzalendoeditor

Katika kuadhimisha Wiki ya Afya Kitaifa, Huduma mbalimbali za Afya ikiwemo upimaji wa macho bure zinatolewa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Wakizungumza mara baada ya kupata huduma mbalinbali ikiwemo upimaji wa macho bure , baadhi ya wananchi hao wameonesha kufurahishwa na huduma hizo huku wakitoa wito kwa wananchi wengine kuchangamkia fursa hiyo muhimu.

Jofrey Mtewele ni mmoja wa wananchi walionufaika na upimaji wa macho bure amevutiwa na huduma zinazotolewa huku akitoa wito kwa wananchi wengine kuchangamkia fursa hiyo ya kuchunguza afya na ushauri bure.

“Nimefurahi sana nimefika na kupatiwa huduma, nimepima macho na hakuna foleni niwasihi na wananchi wengine wajitokeze “amesema.

Dkt. James Shimba ni Daktari Bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando amesema ni muhimu kujenga desturi ya kuchunguza afya ya macho mara kwa mara.

Maadhimisho ya Wiki ya Afya kitaifa yaliyoanza siku ya tarehe 3 – 8, Mwezi 4, 2025 Katika Viwanja vya CCM Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma huduma mbalimbali za Upimaji na Uchunguzi wa awali zinapatikana ambazo ni
1. Upimaji wa Figo
2. ⁠Upimaji wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa
3. ⁠Upimaji wa Shinikizo la Damu (BP)
4. ⁠Upimaji wa Ugonjwa wa Kisukari
5. ⁠Upimaji wa Kifua Kikuu
6. ⁠Upimaji wa Uzito na hali ya lishe
7. ⁠Huduma za Kinywa na Meno
8. ⁠Upimaji na matibabu ya Macho
9. ⁠Huduma za uzazi wa Mpango
10. ⁠Upimaji wa Saratani ya Matiti na Mlango wa Kizazi
11. ⁠Chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi (HPV)
12. ⁠Msaada wa saikolojia na Afya ya Akili
13. ⁠Elimu ya Lishe
14. ⁠Upimaji wa Saratani

Huduma hizi zinatolewa na Watalaamu Bingwa na Bobezi kutoka katika Hospitali za *JKCI, BUGANDO, BENJAMINI MKAPA, UDOM, DODOMA GENERAL HOSPITAL, KIBONG’OTO HOSPITAL, OCEAN ROAD, KCMC, MIREMBE NA MOI*

Muda ni kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni na huduma zote zinatolewa bila malipo na Wiki ya Afya Kitaifa inakwenda sambamba na kaulimbiu isemayo”Tulipotoka, Tulipo, Tunapokwenda, Tunajenga Taifa Imara lenye Afya.

About the author

mzalendoeditor