Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, ASF Thomas Majuto, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, akimpandisha cheo cha Usajini
ZM 3665 CPL – Saidi Issa Saidi kutoka Kituo cha Kazi Kahama
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, ASF. Thomas Majuto, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, amevika vyeo askari watatu wa Mkoa wa Shinyanga kutoka cheo cha Koplo (CPL) hadi Sajini (SGT).
Hafla hii ya kihistoria imefanyika leo katika kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga.
Katika hafla hiyo, askari waliopandishwa cheo ni ZM 3505 CPL – John William Masanja kutoka Kituo cha Kazi Shinyanga, ZM 3600 CPL – Muhaji Juma Mmanga kutoka Kituo cha Kazi Kahama na ZM 3665 CPL – Saidi Issa Saidi kutoka Kituo cha Kazi Kahama
Akizungumza kwenye hafla hiyo, ASF Majuto amesema kuwa, “Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, nimewavika vyeo askari hawa watatu kwa taratibu za kijeshi. Hii ni sehemu ya juhudi za kuenzi na kutambua michango ya askari wetu katika utekelezaji wa majukumu yao. Watumishi hawa ni miongoni mwa askari 435 nchini waliofanikiwa kupandishwa cheo cha Sajini na Koplo wa Zimamoto na Uokoaji kuanzia tarehe 13 Machi 2025.”
“Askari mliopandishwa cheo, nendeni mkatekeleze majukumu yenu kwa ufanisi na bila upendeleo. Mkaoneshe utendaji bora, nidhamu, na kujitolea katika kazi zenu,” ameongeza ASF. Majuto.
Kwa upande wao, askari hao wameeleza furaha yao na shukrani kwa uongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuwaamini na kutambua mchango wao.
Wameahidi kufanya kazi kwa nidhamu, weledi, na kufuata sheria, kanuni na taratibu za Jeshi, huku wakisisitiza dhamira yao ya kuendelea kutoa mchango mkubwa katika utendaji wa kazi.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, ASF Thomas Majuto, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, akimpandisha cheo cha Usajini
ZM 3665 CPL – Saidi Issa Saidi kutoka Kituo cha Kazi Kahama
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, ASF Thomas Majuto, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, akimpandisha cheo cha Usajini
ZM 3600 CPL – Muhaji Juma Mmanga kutoka kituo cha kazi Kahama
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, ASF. Thomas Majuto, kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, akimpandisha cheo cha Usajini
ZM 3505 CPL – John William Masanja kutoka kituo cha kazi Shinyanga
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, ASF. Thomas Majuto akiwa katika hafla ya kuwapandisha cheo cha Usajini askari watatu kutoka Mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, ASF. Thomas Majuto akizungumza wakati wa hafla ya kuwapandisha cheo cha Usajini askari watatu kutoka Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, Mkaguzi Msaidizi Hafidhi Ramadhan Omari akizungumza wakati wa hafla hiyo
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, ASF. Thomas Majuto (wa pili kulia) akiwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliopandishwa cheo ambao ni ZM 3505 CPL – John William Masanja kutoka Kituo cha Kazi Shinyanga, ZM 3600 CPL – Muhaji Juma Mmanga kutoka Kituo cha Kazi Kahama na ZM 3665 CPL – Saidi Issa Saidi kutoka Kituo cha Kazi Kahama
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliopandishwa cheo ambao ni ZM 3505 CPL – John William Masanja kutoka Kituo cha Kazi Shinyanga, ZM 3600 CPL – Muhaji Juma Mmanga kutoka Kituo cha Kazi Kahama na ZM 3665 CPL – Saidi Issa Saidi kutoka Kituo cha Kazi Kahama
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog